1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA:Baraza la Usalama lalainisha vikwazo dhidi ya Iran

23 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCGH

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limefanya mabadiliko kidogo kwenye rasimu ya mapendekezo ya kuwekea vikwazo nchi ya Iran baada ya nchi hiyo kukataa kusitisha mpango wake ya kurutubisha madini ya uranium.Baraza hili linatarajiwa kupiga kura ya kuidhinisha vikwazo hivyo hapo kesho baada kufanya kikao cha siri jana jioni.Mataifa wanachama wa kudumu walio na kura ya turufu katika baraza hilo… Uingereza,Uchina,Ufaransa ,Urusi,Marekani vilevile Ujerumani.

Kulingana na Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa Emyr Jones Parry rasimu hiyo iko tayari kupigiwa kura na wanapanga mkutano wa mwisho hii leo.

Rasimu hiyo inalenga kupiga marufuku nchi ya Iran kutouza silaha katika mataifa ya nje vilevile kuwekewa vikwazo vya biashara.Aidha inaipa nchi ya Iran miezi miwili kutimiza masharti hayo au kuwekewa vikwazo vya kiuchumi bila vya kijeshi.Iran kwa upande wake inashikilia kuwa haibadili msimamo wake na ilianzisha mazoezi ya kijeshi kuonyesha nguvu zake za kujilinda.