1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

UMOJA WA MATAIFA:Baraza la usalama kuidhinisha kuongezwa kwa muda wa UNAMI

10 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBaW

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatarajiwa kuidhinisha azimio la kupanua ujumbe wa Umoja wa Matifa nchini Iraq.Marekani na Uingereza wanaofadhili rasimu ya azimio hilo walichelewesha hatua ya kulipigia kura ili kuipa serikali ya Iraq muda wa kupitia mabadiliko madogo yaliyofanywa. Waziri mkuu wa Iraq Nuri al Maliki yuko katika ziara rasmi nchini Uturuki na Iran jambo lililopelekea kuahirishwa kwa shughuli hiyo kwa siku moja.hayo ni kwa mujibu wa balozi wa marekani katika Umoja wa Mataifa Zalmay Khalilzad.

Azimio hilo linalenga kuongeza muda wa ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini humo UNAMI kwa mwaka mmoja.Ujumbe huo ulitarajiwa kumaliza muda wake hii leo.Hatua hiyo aidha inanuia kumwezesha mjumbe maalum wa Umoja wa mataifa nchini Iraq kushauri,kusaidia vilevile kuunga mkono serikali katika masuala ya kiuchumi,kisiasa na haki za binadamu.Mjumbe huyo anatekeleza majukumu hayo kulingana na mazingira atakayokuwamo.

Ujumbe wa UNAMI uliundwa mwaka 2003 na kuhusisha mamia ya wafanyikazi kutoka mataifa ya kigeni vilevile raia wa Iraq.Umoja wa mataifa ulilazimika kuondoa wafanyikazi wake wengi mjini Baghdad mwaka huohuo baada ya makao yake makuu kushambuliwa kwa bomu lililosababisha vifo vya wafanyikazi 22.