Umoja wa mataifa, New York. Sudan yakataa mpango wa umoja wa mataifa. | Habari za Ulimwengu | DW | 10.03.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Umoja wa mataifa, New York. Sudan yakataa mpango wa umoja wa mataifa.

Rais Omar al-Bashir wa Sudan ameupinga mpango wa kutuma wanajeshi wa kulinda amani wa umoja wa mataifa katika jimbo la Darfur katika barua aliyomwandikia katibu mkuu wa umoja huo , amesema afisa mmoja wa umoja wa mataifa jana Ijumaa.

Msemaji wa katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon, Marie Okabe amesema kuwa katibu mkuu ameipata barua hiyo siku ya Alhamis , karibu miezi mitatu baada ya kumtaka al-Bashir kuonyesha kukubaliana kwake na mpango huo kwa maandishi.

Umoja wa mataifa unataka kuunda jeshi la pamoja la kulinda amani litakalokuwa na wanajeshi wapatao 22,000 kati ya umoja wa Afrika na umoja wa mataifa katika jimbo la Darfur.

Al-Bashir alikubaliana na mpango huo Novemba mwaka jana , lakini amekuwa akibadilisha msimamo wake kila mara hivi karibuni .

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com