Umoja wa mataifa, New York. Panama ndani ya baraza la usalama. | Habari za Ulimwengu | DW | 04.11.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Umoja wa mataifa, New York. Panama ndani ya baraza la usalama.

Panama imechaguliwa kuiwakilisha Marekani ya kusini katika baraza la usalama la umoja wa mataifa kuazia Januari mwakani.

Kundi la mataifa ya Marekani ya kusini na Karibik katika umoja wa mataifa , jana kwa kauli moja yaliidhinisha Panama kuwa chaguo lao katika kiti ambacho si cha kudumu katika baraza hilo ambacho kinaachwa na Argentina hapo Desemba 31.

Baraza kuu la umoja wa mataifa mwezi uliopita liipigia kura Ubelgiji, Itali , Afrika kusini na Indonesia kuchukua nafasi ya mataifa mengine manne yanayoondoka katika baraza hilo.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com