Ulaya yakumbwa na mafuriko na joto kali | Wafanyakazi wa Idhaa ya Kiswahili | DW | 22.07.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Timu Yetu

Ulaya yakumbwa na mafuriko na joto kali

Nchi za Ulaya ya Kati na Magharibi,zimeathirika vibaya baada ya mvua kali zilizonyesha, kusababisha mafuriko.Hali ya hatari imetangazwa katika maeneo mengi ya jimbo la Bavaria,kusini mwa Ujerumani.Baadhi ya maeneo,yamezama katika maji yenye kima cha mita moja.

David Cameron,kiongozi wa chama cha upinzani cha Conservative nchini Uingereza akitembelea jimbo lake la uchaguzi lililoathirika kwa mafuriko.

David Cameron,kiongozi wa chama cha upinzani cha "Conservative" nchini Uingereza akitembelea jimbo lake la uchaguzi lililoathirika kwa mafuriko.

Uingereza nayo imeshuhudia mafuriko mabaya kabisa kwa mara ya pili,katika kipindi cha mwezi mmoja. Mamia ya watu katika wilaya ya Worcestershire, walilazimika kuondoka makwao.

Helikopta za kijeshi zimewaokoa zaidi ya watu 100 walionasa kwenye mafuriko,tangu mvua kubwa kuanza kunyesha siku ya Ijumaa.Waziri Mkuu wa Uingereza,Gordon Brown ameahidi kupeleka misaada zaidi katika maeneo yaliyoathirika.

Kwa upande mwingine,idadi ya watu waliokufa kutokana na wimbi la joto kali nchini Rumania,Austria na Bulgaria imefikia 18.Joto kali la juma moja,limeathiri nchi,kuanzia Hungary hadi Ugiriki inayoshuhudia msimu wa joto kali kabisa,tangu zaidi ya karne moja.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com