1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa wazuru Kongo

Josephat Nyiro Charo16 Aprili 2010

Lengo la ziara hiyo ni kuratibu mchakato wa kuondoka wanajeshi wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, MONUC

https://p.dw.com/p/MyYH

Ujumbe wa baraza la usalama la umoja wa mataifa unaoongozwa na balozi wa ufaransa kwenye umoja huo, Gérard Araud kesho unatarajiwa kuwasili Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo kwa ziara ya siku mbili ili kujadiliana na viongozi wa Kongo kuhusu muda wa kikosi cha MONUC kuendelea kubaki nchini humo na taratibu za kuondoka kwake. Kongo tayari imesema kikosi cha MONUC lazima kiondoke katika kipindi cha mwaka mmoja.

Mwandishi wetu wa Kinshasa, Salehe Mwanamilongo ametutumia taarifa ifuatayo:

Insert:

Mtayarishaji: Salehe Mwanamilongo

Mpitiaji: Grace Patricia Kabogo

Mhariri: Sekione Kitojo