1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani yapeleka mitambo ya kusafisha maji Pakistan

27 Agosti 2010

Shirika la misaada ya kifundi la Ujerumani THW, linapeleka Pakistan, tume ya wataalamu na mitambo miwili ya kusafisha maji.

https://p.dw.com/p/OxQ4
Flood victims hang on a rope as they flee the flooded areas in Shikarpur, Sindh province Pakistan on 16 August 2010. More than 1500 people across Pakistan have been killed and hundreds of thousands stranded due to flash floods triggered by the ongoing spell of monsoon rains. The worst floods the country has faced in several decades washed away millions of hectares of crops, submerged villages and destroyed roads and bridges in the north-western province of KhyberPakhtunkhwa, parts of the Pakistan-administered Kashmir region and the eastern province of Punjab. EPA/NADEEM KHAWER
Wahanga wa mafuriko wakiyakimbia mafuriko katika wilaya ya Sindh.Picha: picture-alliance/dpa

Wasaidizi hao watawapatia wahanga wa mafuriko nchini Pakistan, maji safi ya kunywa.Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere mjini Berlin alisema kuwa mitambo hiyo inaweza kusafisha lita 12,000 za maji kwa saa na itawekwa katika wilaya ya Punjab iliyoathirika vibaya.

Bundeskanzlerin Angela Merkel (CDU) gestikuliert am Montag, 23. August 2010, vor der Sitzung des CDU-Vorstands in Berlin. (apn Photo/Berthold Stadler)
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Wakati huo huo Kansela wa Ujerumani Angela Merkel ametoa mwito katika televisheni ya Ujerumani kuhimiza michango ya kuwasaidia wahanga wa mafuriko nchini Pakistan.Hadi sasa,serikali ya Ujerumani imeahidi kutoa msaada wa Euro milioni 25.

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, hivi sasa nchini Pakistan,kiasi ya watu milioni tatu na nusu hawana maji safi ya kunywa.

Mwandishi: P.Martin/ZPR