1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Baerbock akutana na kufanya mazungumzo na Cameron

Sylvia Mwehozi
8 Machi 2024

Ujerumani na Uingereza zinalenga kuimarisha ushirikiano ndani ya jumuiya ya NATO. Hayo yameelezwa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock mara baada ya kukutana na mwenzake wa Uingereza David Cameron.

https://p.dw.com/p/4dI5X
David Cameron | Annalena Baerbock | Berlin
Waziri wa mambo ya nje wa Uingereza David Cameron na mwenyeji wake Annalena Baerbock mjini Berlin Picha: Markus Schreiber/AP Photo/picture alliance

Ujerumani na Uingereza zinalenga kuimarisha ushirikiano ndani ya jumuiya ya NATO. Hayo yameelezwa na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Annalena Baerbock mjini Berlin mara baada ya kukutana na mwenzake wa Uingereza David Cameronhuku vita vya Ukraine vikiingia mwaka wake wa tatu na kabla ya uchaguzi wa Marekani.

Baerbock alisema kuwa kuimarishwa kwa ushirikiano wa kiusalama na kiulinzi kati ya nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kila mara kunamaanisha ushirikiano ndani ya NATO.

Kwa upande wake, Cameron amesema washirika wa Ulaya wanapaswa kuzingatia kuonyesha mshikamano katika maandalizi ya uchaguzi wa Marekani, bila kujali kama walijiondoa ndani ya Umoja wa Ulaya mnamo 2020.

Baerbock na Cameron walikutana kwenye hafla ya pili ya mazungumzo ya kimkakati kati ya nchi hizo mbili haswa ushirikiano kwenye sera ya mambo ya nje.