1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani kuweka masharti magumu ili kuzuia uhamiaji

7 Novemba 2023

Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz ameafikiana na viongozi wa majimbo yote 16 nchini humo kuwepo kwa masharti magumu zaidi ya kuzuwia idadi kubwa ya wahamiaji kuingia Ujerumani.

https://p.dw.com/p/4YVef
Berlin Bund-Länder-Treffen im Bundeskanzleramt
Kansela wa Ujerumani Olaf Scholz akiwa na mawaziri viongozi wa majimbo ya UjerumaniPicha: Bernd von Jutrczenka/dpa/picture alliance

Muafaka huo umepatikana mjini Berlin katika jambo ambalo limekuwa tatizo kubwa la kisiasa na kijamii.

Hatua hizo mpya zitajumuisha msaada wa kifedha kwa majimbo ili kukabiliana na suala la uhamiaji pamoja na kuharakisha mchakato wa kuomba hifadhi nchini Ujerumani.

Scholz ambaye amekuwa akikabiliwa na shinikizo kutoka kwa upinzani, ameyaelezea makubaliano hayo kuwa ya kihistoria.

Hadi mwishoni mwa mwezi Septemba, idadi ya waomba hifadhi imeongezeka nchini Ujerumani kwa asilimia 73 ukilinganisha na kipindi hicho mwaka uliopita.

Ujerumani imewapokea pia Waukraine zaidi ya milioni 1 tangu Urusi ilipoanzisha uvamizi wake nchini humo.