1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani hatarini kupoteza sifa ya utengenezaji magari

Saumu Mwasimba
4 Septemba 2023

Ujerumani iko katika hatari ya kupoteza sifa yake ya kuwa nchi yenye nguvu kubwa katika sekta ya utengenezaji magari.

https://p.dw.com/p/4Vv63
Zwickau Autofabrik | Volkswagen ID.3
Moja ya kiwanda cha utengenezaji magari UjerumaniPicha: Sean Gallup/Getty Images

Hayo yameelezwa na rais wa chama cha sekta ya utengenezaji magari cha Ujerumani VDA,Hildegar Müller ambaye amesisitiza kwamba japokuwa makampuni ya utengenezaji magari nchini Ujerumani watanusurika,nchi hiyo haitoweza kubakia na sifa yake kama kitovu cha utengenezaji magari,bila ya kufanyika mageuzi makubwa.

Soma pia:Teknolojia ya Akili bandia huenda ikasababisha ubaguzi

Müller ametowa mtazamo huo kabla ya maonesho makubwa ya biashara ya  magari IAA yanayofanyika mjini Munich.

Miongoni mwa sababu kubwa alizozitaja kuchangia matatizo,ni kuwepo kwa kasi ndogo ya maamuzi ya kisiasana mpango wa kisheria kwaajili ya kusimamia masuala kama teknolojia ya akili bandia.