1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ujerumani haitashiriki vita Syria

Sekione Kitojo
12 Aprili 2018

Kansela  wa  Ujerumani Angela Merkel amesema shambulio la gesi ya sumu linalodaiwa kufanywa na serikali ya Syria linadhihirisha  utawala wa rais Bashar al-Assad umeshindwa kutokomeza hazina yake ya silaha za sumu.

https://p.dw.com/p/2vwuS
Merkel empfängt dänischen Ministerpräsidenten Rasmussen
Picha: picture-alliance/dpa/W. Kumm

Rais  wa  Marekani Donald Trump amesema  kwamba shambulio  dhidi  ya  Syria  huenda  likafanyika "hivi  karibuni  ama hata  sio  hivi  karibuni  kabisaa"  akidai  kwamba  hajawahi kuashiria muda  wa  kujibu  shambulio  hilo la  gesi  ya  sumu , suala aliloonesha  ishara kwamba lingefanyika hivi  karibuni. 

Kansela  wa  Ujerumani  amesema ," tunapaswa  kukiri  kwamba  ni dhahiri  hatua  za  kuharibu  silaha  hizo  za  sumu  haikufanyika kwa ukamilifu," alisema , sio  kwamba  hakuna  ushahidi  wa  kutosha kwamba  serikali  ya  Syria  ilitumia  silaha  hizo  za  sumu.  Serikali ya  Syria  iliepuka  mashambulizi  ya  Marekani  na  Ufaransa mwaka 2013 katika  kujibu  shambulio  linaloshukiwa  kuwa  ni  la gesi  ya  sarin  kwa  kukubali  kukabidhi  hazina  yake  ya  silaha  za sumu.

President Trump comments on Syria, FBI raid of Michael Cohen's office at White House
Rais wa Marekani Donald TrumpPicha: picture alliance / Newscom

Kufuatia  madai  ya  matumizi  ya  gesi  ya  sumu  katika  eneo lililokuwa  linashikiliwa  na  waasi  la  Douma, rais  wa  Marekani Donald Trump  wiki  hii aliongeza  mbinyo  dhidi  ya  Damascus , akionya  katika  maandishi  yake  kadhaa  katika  mtandao  wa kijamii  wa  Twitter kwamba "makombora yanakuja" ili  kulipiza  kisasi. Msemaji wa  serikali  ya  Urusi Dmitry Peskov  hata  hivyo amesema  Urusi  inafuatia  kwa  karibu  taarifa  zinazotoka Marekani.

"Urusi  inafuatilia  kwa  karibu  matamshi  kutoka  Marekani  na  bado tunaamini kwamba  ni  muhimu  sana  kuepuka  hatua  zozote ambazo zitaweza  kusababisha msuguano nchini Syria. Tunafikiri  hali  hiyo italeta  athari  mbaya  katika  mchakato mzima wa utulivu wa  Syria."

Ujerumani haitashiriki vita

Kansela  wa  Ujerumani  angela  Merkel  amesema "hatua  kadhaa " zitatiliwa  maanani  kujibu  shambulio  hilo  la  gesi  ya  sumu, lakini aliondoa  uwezekano  wa  hatua  za  kijeshi. Ujerumani  haitashiriki kijeshi, lakini itatoa msaada  iwapo wawakilishi  katika  baraza  la Usalama  la  Umoja  wa  mataifa , wataamua  kuchukua  hatua  mbali na  hatua  za  kidiplomasia"  alisisitiza.

Hamburg G20 Angela Merkel und Donald Trump
Rais Donald Trump wa Marekani (kushoto) akizungumza na Angela Merkel wa UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa/M. Kappe

Ufaransa  lakini  inatarajiwa  kujiunga  na  Marekani  na  Uingereza kufanya  mashambulio  ya  anga  ama  njia  nyingine  za mashambulio  kujibu shambulio  hilo  la  silaha  za  sumu , lakini inabaki  bila  uhakika  iwapo  hilo huenda  likatokea  ama  hata iwapo kweli  litatokea.

Rais Emmanuel Macron wa  Ufaransa  amesema  leo  kwamba  nchi yake inaushahidi  kwamba  serikali  ya  Syria  ilifanya  shambulio hilo  la  silaha  za  sumu wiki  iliyopita  na  itaamua  iwapo ishambulie wakati taarifa  zote  muhimu litakapokuwa  zimekusanywa.

"kuna mfumo  wa  sheria  za  kimataifa, tuna ushahidi  kwamba  wiki iliyopita  shambulio  la  gesi  ya  sumu  ya  klorine  lilifanyika na kwamba   lilifanywa  na  serikali  ya  Bashar al-Assad. Sheria  za kiutu  na kutoa  nafasi  kwa  misaada  ya  kiutu, kusaidia  asasi zisizo za  kiserikali  kuwasaidia  watu ndani  ya  nchi  hiyo, katika njia  kwenda  Idlib na  kuwatoa  raia  kutoka  katika  eneo  hilo. Watoto  pamoja  na  wanawake.  Ili  kutoona  tena  picha  za  kutisha za  uhalifu  ambapo  tuliona  watoto  na  wanawake  wakifariki kutokana  na  kushindwa kupumua."

Belgien EU-Gipfel - Emmanuel Macron
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron Picha: Reuters/F. Lenoir

Rais  wa  Marekani  Donald Trump ameandika  katika  ukurasa  wa Twitter leo  asubuhi, "Sijasema  lini shmabulio dhidi  ya  Syria litafanyika. Huenda  ni  hivi  karubuni ama  hata  pengine sio  hivi karibuni kabisa !" wakati  huo  huo meli  za  kijeshi  za  Urusi zimeondoka  kutoka  katika  vituo vyake  katika  bahari  ya Mediterania  kwa  kile  kilichoelezwa  kuwa ni  usalama  wake, hali iliyoelezwa  na makamu  mwenyekiti  wa  kamati  ya  ulinzi  ya  Urusi kwamba  ni  hatua  za  kawaida , wakati  kuna  kitisho cha shambulio.

Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre / afpe

Mhariri:  Iddi   Ssessanga