1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uhaulishaji wa sheria za Ujerumani

14 Aprili 2011

"Tunaaminika, ni rahisi na tunatabirika." Hivi ndivyo Ujerumani inavyotangaza juu ya kuuza mfumo mzima wa sheria zake.

https://p.dw.com/p/10tRx
Picha: Fotolia/rupbilder

Lengo la tangazo hilo liko wazi. Ni kuyavutia makampuni ya nje kuukumbatia mfumo wa sheria wa Ujerumani, kupewa unafuu kwa makampuni ya Ujerumani katika nchi za nje, kuimarisha biashara na hata taifa kwa jumla. Kuipigia debe sheria ya Ujerumani kuna lengo maalum.

Justizministerin Sabine LEUTHEUSSER-SCHNARRENBERGER FDP
Waziri wa Sheria wa Ujerumani Sabine Leutheusser SchnarrenbergerPicha: picture-alliance/Sven Simon

Wakati mwingine ufanisi wa Ujerumani hauisaidii kama nchi. Inapotokea wakati kwamba kifungu cha sheria ya Ujerumani nambari 19 kinatakiwa kuweka sawa kikanuni jambo moja, kwa Ufaransa itahusu mambo mawili, kwa China sheria hiyo haitowezekana kabisa, anasema Knut Pisler kutoka taasisi ya kimataifa inahusika na masuala ya sheria binafsi ya nchi za nje ya Max-Planck ambaye binafsi anahusika zaidi na masuala ya sheria ya China. Anasema sheria ya Ujerumani nchini China ina nafasi kubwa lakini ameongeza kusema kwamba, watunga sheria nchini China hawazingatii mifumo ya sheria za nchi zingine bali unatazama mifumo mbali mbali ya sheria na kulinganisha na baadae kuamua ni upi unaoendana na hali halisi ya taifa lao. Mtu hawezi kusema kwamba taasisi fulani ya sheria kutoka Ujerumani au Ufaransa inaweza kufikiriwa kutumiwa na nchi hiyo.

Baadhi ya nchi katika miaka ya nyuma zimewahi kuchukua takriban sehemu nzima ya mfumo wa sheria ya Ujerumani, mfano ni sheria ya uhalifu ya Uturuki na uendeshwaji wa kesi za uhalifu, pia Ugiriki na Ureno zinafuata sehemu ya sheria ya Ujerumani katika sheria zake za kiraia. Baadhi ya sheria za Japan pia zimefuata mfumo wa sheria za Ujerumani.

Aidha barani Afrika mfumo wa sheria za Ujerumani hadi sasa hauna nafasi kubwa. Kimsingi katika bara hilo nyingi ya sheria zake zinazingatia mfumo wa Ukoloni. Chuo kikuu cha Würzburg kimeanzisha mradi unaweza kubadilisha hali hiyo. Karin Linhart ni mawalimu wa masomo ya sheria za Ujerumani na Ulaya katika chuo kikuu cha Kinshasa, lengo likiwa kwa upande mmoja ni kutoa ujuzi wa Ujerumani nchini Kongo lakini upande mwingine mbali na utalaamu miradi ya aina hiyo ni sehemu ya msaada wa maendeleo, kwa sababu Ujerumani pia ina masilahi ya kutaka ushirikiano. Kwa upande huo kwa hivyo panahitajika mazingira mazuri ya uwekezaji na kuyaboresha mazingira hayo ni jambo muhimu.

Bundesverfassungsgericht Dossierbild 3 NEU
Mahakimu wa mahakama ya katiba ya UjerumaniPicha: picture-alliance/dpa

''Ni vizuri ikiwa sheria zitazingatiwa, kukiwa na uwazi na ikiwa watakuwa na ufahamu mzuri wa sheria zetu. Hii ina maana kwamba wawekezaji watakuwa na uwezekano wa uhakika kuwekeza nchini Kongo, kwa kuona vipengele vya sheria ambavyo wanavifahamu. Na hali hiyo inajenga hali ya kuaminiana zaidi,'' anasema Linhart.

Ama kwa upande mwingine mwalimu huyo wa masuala ya sheria amezungumzia kuhusu katiba katika nchi ambazo mahakama kuu ndiyo inayotoa uamuzi wa mwisho kisheria. Nchi za Asia na hata za Ulaya ya Kusini mashariki zinazingatia zaidi sheria na baadhi ya vifungu vya sheria ya Ujerumani linapokuja suala la katiba. Uhispania, Ureno na Hungary ni mifano tu ya nchi ambazo mahakama zake za katiba zimefuata mfumo wa mahakama kuu ya katiba ya Ujerumani.

Mwandishi: Grathwohl Daphne ZR/Saumu Mwasimba

Mhariri: AbdulRahman.