Nchini Tanzania bado uhaba wa mafuta unashuhudiwa jijini Dar es salaam,baada ya vituo vingi vya uuzaji bidhaa hiyo kuendelea kufungwa na vingine vikifungua lakini havina mafuta ya kuuza.
Uhaba wa mafuta nchini Tanzania
Hatua hii inajitokeza baada ya serikali kutoa agizo wiki hii kuwataka wauzaji wa bidhaa hiyo wafungue vituo vyao au wafutiwe leseni.Misururu ya magari bado inasemekana kuonekana katika vituo vichache vilivyofunguliwa.Aidha hali sio ya kawaida katika vituo hivyo kama alivyotueleza mmoja wa wamiliki wa vituo kadhaa vya mafuta katika jiji la Dar es salaam .
Mwandishi: Saumu Mwasimba
Mhariri:AbdulRahman