1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Ugiriki yaomba msaada kutoka Ulaya na IMF

24 Aprili 2010

Serikali ya Ugiriki inayokabiliwa na kitisho cha kufilisika, imeomba msaada kutoka kwa washirika wenzake katika kanda inayotumia sarafu ya Euro na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF.

https://p.dw.com/p/N5FS
Greek Finance Minister George Papaconstantinou speaks during a media conference after a meeting of EU finance ministers in Madrid, on Saturday, April 17, 2010. European Union finance ministers were working Saturday on ways to ensure tougher banking supervision, and considering a bank levy to pay for banks that collapse in the future, hoping to prevent a repeat of the recent financial crisis which cost governments billions of euros. (AP Photo/Virginia Mayo)
Waziri wa Fedha wa Ugiriki, Geoerge Papaconstantinou.Picha: AP

Waziri wa Fedha wa Ugiriki, George Papaconstantinou amesema msaada wa fedha kutoka nchi za kanda ya Euro na shirika la fedha la kimataifa , IMF upo njiani lakini utachukua siku kadhaa kabla ya kufika nchini humo.

Siku ya Ijumaa, Ugiriki ilitoa ombi kwa Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF, kuipatia msaada wa Euro bilioni 45 ili iweze kulipa madeni yake makubwa.

Lakini Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel amesema, kuna masharti ya kutimizwa. Kwanza, mpango unaoaminika kupunguza matumizi, ujadiliwe kati ya Ugiriki, Kamisheni ya Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa. Pili, mpango huo utakapowasilishwa, basi Kamisheni ya Ulaya, Benki Kuu ya Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa lazima zitathmini ikiwa hali ya sarafu ya Euro inalazimisha kuisaidia Ugiriki."

German Chancellor Angela Merkel delivers a speech at the German Federal Parliament in Berlin, Germany, Thursday, April 22, 2010. (AP Photo/Michael Sohn)
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Baada ya kutimizwa kwa masharti hayo mawili, masuala mengine kuhusu kiwango na njia ya kutoa msaada huo yanaweza kujadiliwa.

Mwandishi:Moss,Peter/RTRE/AFP

Mhariri:Martin,Prema