Ufaransa na Libya -gharama ya ukombozi ? | Matukio ya Kisiasa | DW | 03.08.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Ufaransa na Libya -gharama ya ukombozi ?

Ufaransa iliafikiana mapatano gani na Libya hadi wauuguzi wa Bulgaria wakatoka korokoroni na kurudi nyumbani ? Biashara ya silaha na kumvalisha gadafi joho safi.

Ilikuwa furaha ilioje kuachiwa kwa wauuguzi wa kibulgaria kutoka gerezani nchini Libya na kurudi nyumbani.Punde si punde lakini, swali lilizuka ni gharama gani ililipwa nah ii ikaweka kivuli chake juu ya furaha hiyo.

Wazi ni kuwa, rais Nocholas Sarkozy wa Ufaransa, amejiamulia peke yake na zaidi amefungamkataba na Muamar gadhafi kumuuzia silaha.Kibiashara, Sarkozy hapo ametamba,lakini kiadilifu je ?

Kama hana la kusema namna hivi hakuonekana rais wa Ufaransa tangu kushika madaraka.Je, rais Sarkozy, alieparamia kilele cha madaraka kwa kujitapa angeivika siasa ya nje ya Ufaransa nguo ya uadilifu ana hisia mbaya zinazomtaabisha ?

Haoneshi yutayari kuweka bayana mapatano aliyofunga na Gadafi.Yabainika anataka kuacha ukweli ujidhihirishe binafsi na unadhhirika na motto wa Gadafi-Saif anafunua kawa:

Sio tu Ufaransa itaiuzia libya kinu cha kinuklia cha kugeuza maji ya chumvi ,bali pia itaiuzia makombora 100 ya kujikinga na vifaru kwa kima cha Euro milioni 100.Isitoshe, Ufaransa,amefichua itaijengea Libya kiwanda cha silaha.

Kama usemi usemavyo-mkonomtupu haurambwi:

Kwahivyo, rais Sarkozy na waziri wake wa nje kutoka chama cha kisoshalisti, Bernard Kouchner

Wanakanusha kwamba biashara hiyo haina uhusiano kabisa na maafikiano ya kuachwa huru wauuguzi wa kibulgaria na daktari wa kipalestina na pia hakujachangiwa kwa aina yoyote na heba ya mke wa Sarkozy- Cecilia.

Kanali Gadafi ataka kujigeuza kutoka Kiongozi alielaaniwa na kuwekwa kando ageuke wa kuheshimiwa na kupokewa.Na rais sarkozy,amemvika sasa joho hilo jipya.Na amemfanyia hata mengi zaidi.

Hawajali iwapo hadi karibuni,Gadafi akitaka kuunda silaha za kuhilikisha umma na maajenti wake walituhumiwa kuhusika na kuripua ile ndege yxa Pan Am juu ya anga la Lockerby na mwishoni, ikiwatesa wafungwa wake wauuguzi kutoka Bulgaria korokoroni.

Sarkozy aliahidi kupigania kuwakomboa wabulgaria hao na ahadi hiyo ameitimizalakini kwa gharama ya kumtakasa kiongozi wa utawala wenye shaka-shaka.

Kwa kupeana mikono na Gadhafi,zimetoka mahala pasipojulikana dala milioni 460 kama fidia ya watoto walioambukizwa virusi vya UKIMWI, uwezekano wa kuachwa huru yule jasusi wa Libya alietuhumiwa kuhusika na mripuko wa Lockerby.Na hii imewakomboa wauguzi.

Kiokosi hicho ni halali ?-ndio matokeo yake ni mazuri,lakini njia iliotumika ni ovu.Na ikiwa hakuna cha kuficha,kwanini basi rais Sarkozy wa Ufaransa amenyamaa kimya hajibu mashtaka ?

Bila shaka yafaa kusaka njia ya kuirejesha libya katimka ukoo wa kimataifa unaoheshimika,lakini mtu afanye hivyo kwa ushirikiano na wenzake katika Umoja wa Ulaya .Na ni hapo Srakozy,anasubiriwa kujibu ilikuaje .

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com