Uchumi wa Ujerumani wakua zaidi.
14 Agosti 2010Matangazo
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Ofisi ya Takwimu mjini Wiesbaden, pato la ndani la Ujerumani limeongezeka kwa asilimia 2.2 ukilinganisha na robo ya kwanza ya mwaka huu.
Hali hiyo imefanya kukua kwa uchumi kwa kiasi kikubwa tokea kuunganika tena kwa Ujerumani miaka 20 iliyopita.
Mkuu wa kitengo cha uchumi katika kampuni ya uwekezaji ya DekaBank, Holger Bahr amesema ukuaji huo umetokana sana na usafirishaji wa bidhaa nje na uwekezaji.
Aidha Pato la ndani la Ufaransa pia limeongezeka kwa asilimia 0.6 kwa kipindi cha miezi minne iliyopita, huku Uhispania uchumi wake ukiongezeka kwa asilimia 0.2.