1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Tanzania

6 Novemba 2010

Rais Kikwete ameapishwa kuiongoza Tanzania kwa mara nyenginbe tena.

https://p.dw.com/p/Q0O3
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete.Picha: AP Photo

Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete ameapishwa rasmi hii leo kuiongoza nchi hiyo katika kipindi cha pili cha miaka mitano, baada ya kuchaguliwa tena kuwa rais wa nchi hiyo.

Tansania Sansibar Wahlen Wahlkampf CCM Jakaya Kikwete
Rais Jakaya Kikwete alipokuwa katika kampeni za uchaguzi.Picha: AP

Tume ya Uchaguzi ya Taifa-NEC ilitangaza matokeo hapo jana ambapo ilisema Rais Kikwete ameshinda kwa kupata asilimia 61 ya kura, katika uchaguzi uliofanyika Jumapili iliyopita.

Hata hivyo, kiongozi wa upinzani kutoka chama cha Demokrasia na Maendeleo-Chadema, Dr. Wilbrod Slaa anataka kura zihesabiwe tena kwa madai kuwa kulifanyika udanganyifu. Chama tawala cha Rais Kikwete cha CCM, kimekuwa madarakani tangu Tanzania ilipopata uhuru wake mwaka 1961.

Mwandishi Maryam Abdalla/dpae,rtre

Mhariri:Dahman Mohammed