1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Uchaguzi Senegal waelekea duru ya pili

Admin.WagnerD27 Februari 2012

Matokeo ya awali katika uchaguzi wa Jumapili nchini Senegal, yanamuonyesha Abdoulaye Wade na mpinzani wake wa karibu, Macky Sall, wakikaribiana na kuashiria uwezekano wa duru ya pili ya uchaguzi

https://p.dw.com/p/14AaS
Rais wa Senegal Abdoulaye Wade
Rais wa Senegal Abdoulaye WadePicha: Reuters

Matokeo hayo ya hivi karibuni ambayo yamethibitishwa na msemaji wa Rais Wade yanaonyesha Kiongozi huyo mkongwe mwenye umri wa miaka 85 kuwa na kati ya asilimia 34 na 36, huku mpinzani wake wa karibu Macky Sall akikadiliwa kuwa na kati ya asilimia 32 na 34.

Msemaji huyo anakiri kuwa kwa sasa lazima uchaguzi huo uingie katika duru ya pili kwani rais Wade na Macky Sall ndiyo wanaonekana kushindana kwa karibu sana.

Hali ya matokeo ya Uchaguzi huo inaonekaa kuwa mbaya zaidi kwa Rais Wade kwani taarifa zisizo rasmi zinabainisha kuwa mzee huyo amefanya vibaya hata kwenye Wilaya yake aliyozaliwa.

Bango la Macky Sall ambaye anamnyemelea kwa karibu Wade
Bango la Macky Sall ambaye anamnyemelea kwa karibu WadePicha: DW/D.Köpp

Wakati wa kampeni za uchaguzi huo Rais Wade aliwaambia wa Senegali kuwa kwa sasa anahitaji wakati mwingine Zaidi ili kuweza kumalizia mipango yake ya kuwaletea maendeleo Wasenegali .

Huku akijigamba kuwa katika utawala wake aliweza kuwajengea barabara bora, viwanja vya ndege lakini nao wapinzani wake wakimkosoa kwa majigambo hayo wakisema Wade alishindwa kabisa kuyaborosha maisha ya Wasegali wa kawaida.

Ushindani katika matokeo hayo ulianza kuonekana mapema kwani matokeo ya awali yalionyesha kuwa Wade alikuwa akiongoza kwa asilimia 24 na Sall alikuwa na asilimia 21 na haya yalikuwa ni kwa asilimia 10 ya kura zilizohesabiwa hapo awali.

Kampeni ya uchaguzi iligubikwa na ghasia
Kampeni ya uchaguzi iligubikwa na ghasiaPicha: AP

Taswira hiyo hiyo bado inazidi kuonekana kwa matokeo haya ya Taifa hili linalongozwa Kwa sasa na Kiongozi mwenye umri wa miaka 85. Hali hii ya umri wake akilinganishwa na wagombea wengine ameonekana kuwa ni mtawala anayeng'ang'ania madaraka.

Johnnie Carson ambaye ni mjumbe wa Wizara ya mambo ya nje ya Marekani anayeshughulikia Afrika anakili kuwa uchaguzi huo wa Senegali umefanyika kwa amani na utulivu.

Wadadisi wanaashiri kwamba ikiwa uchaguzi wa jana utaingia duru ya pili , itakua ni hali ngumu kwa rais wade ambaye ameshaliongoza taifa hilo kwa miaka 12.

Vibonzo vimekuwa vikichorwa na kumuonyesha Marck Sall kuwa mshindi wa Urais hilo , mtu makini na mwenye nguvu kuliko Wade anayeonekana kuwa mkongwe mno.

Mjumbe wa Umoja wa Afrika katika uchaguzi huo Rais Mstaafu wa Nigeria Olusegun Obasanjo amesema amefurahishwa na namna jimnsi zoezi zima la uchaguzi lilivyofanyika.

Uitikiaji wa wapiga kura ulikuwa wa kuridhisha
Uitikiaji wa wapiga kura ulikuwa wa kuridhishaPicha: Reuters

Senegal , taifa lililokuwa koloni la Ufaransa lilipata uhuru wake 1960

na limekuwa likisifiwa kwa kuheshimu demokrasia ikilinganishwa na mataifa mengine jirani katika eneo hilo la Afrika magharibi. Hata hivyo uamuzi wa Rais wade kuibadili katiba ili kugombea tena kwa mhula wa tatu, umelitia doa taifa hilo na kuzusha wasiwasi wa kuhujuma mafanikio ya kidemokrasi yaliopatikana.

Mwadishi :Adeladius Makwega

Mhariri: Mohammed Abdul-Rahman