Senegal kupiga kura leo | Matukio ya Kisiasa | DW | 26.02.2012
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Matukio ya Kisiasa

Senegal kupiga kura leo

Uchaguzi unafanyika leo nchini Senegal, uchaguzi ambao umekumbwa na vurugu wakati wa kampeni , ambapo juhudi za rais Abdoulaye Wade za kuwania kipindi cha tatu cha utawala zimezusha maandamano yaliyomwaga damu.

Der Praesident des Senegals, Abdoulaye Wade, steht bei einer Wahlkampfveranstaltung in Dagana, Senegal (Foto vom 10.02.12). Die Praesidentschaftswahl im westafrikanischen Senegal ist fuer den 26. Februar 2012 angesetzt. (zu dapd-Text) Foto: Gabriela Barnuevo/AP/dapd // Eingestellt von wa

Rais wa sasa wa Senegal Abdoulaye Wade

Koloni hilo la zamani la Ufaransa ni moja kati ya nchi ambazo zimekuwa mstari wa mbele katika kuanzisha demokrasia katika bara la Afrika, ikijivunia chaguzi mbali mbali bila kizuwizi tangu kupata uhuru mwaka 1960. Ni taifa pekee katika eneo la Afrika magharibi ambayo haijakumbwa na mapinduzi ya kijeshi.

Hata hivyo juhudi za rais Wade za kuwania kipindi cha tatu cha utawala kinaonekana kuwa mtihani mgumu kwa sifa ya kidemokrasia ya Senegal , na kusababisha wasi wasi wa kimataifa baada ya wiki kadha za maandamano ambayo yamesababisha watu sita kuuwawa.

Takriban watu milioni 5.3 wamejiandikisha kupiga kura hii leo.

Wade anakabiliwa na wagombea 13 wa kiti cha urais ikiwa ni pamoja na mawaziri wakuu watatu wa zamani , Idrissa Seck, Macky Sall , Moustapha Niasse na kiongozi wa chama cha kisoshalist Ousmane Tanor Dieng. Hakuna ambaye amejitokeza kuwa na nafasi ya mbele dhidi ya Wade.

licha ya kutumikia vipindi viwili madarakani, muda ambao aliuanzisha binafsi, Wade amesema mabadiliko ya katiba ya mwaka 2008 yanayorefusha kipindi cha uongozi hadi miaka saba yanamruhusu kutumikia vipindi vingine viwili.

Kiongozi mkongwe Afrika

Akiwa kiongozi wa pili katika bara la Afrika mwenye umri mkubwa baada ya kiongozi wa Zimbabwe Robert Gabriel Mugabe mwenye umri wa miaka 88, Wade amesema anahitaji muda zaidi kumaliza mradi wake mkubwa . Lakini ameshutumiwa kwa kutaka kumuweka mtoto wake wa kiume Karim Wade kama mrithi wake.

Ujumbe wa ngazi ya juu wa amani kutoka umoja wa Afrika ukiongozwa na rais wa zamani wa nigeria Olusegun Obasanjo umependekeza kuwa iwapo Wade atashinda , atastaafu baada ya miaka miwili.

Re-elected President Olusegun Obasanjo smiles as he leaves a ceremony where he was presented with a certificate of return by the Independent National Electoral Commission at the INEC headquarters in the Nigerian capital Abuja Wednesday, April 23, 2003. (AP Photo/Ben Curtis)

Rais wa zamani wa Nigeria Olusegun Obasanjo, ambaye ameongoza ujumbe wa amani wa AU nchini Senegal

Si Wade wala upande wa upinzani ambao umekubali mapendekezo hayo.

Kundi la Juni 23

Kundi linalojulikana kama vuguvugu la Juni 23, ambalo ni muungano wa vyama vya upinzani na wanaharakati , limetoa wito siku ya Jumamosi kwa uchaguzi wa rais kutayarishwa katika muda wa miezi sita hadi tisa , ambapo Wade hatashiriki. Kampeni ya kumpinga Wade ilifanywa na kundi la wanamuziki wa rap, wagombea wa kiti cha urais, wanaharakati na mwanamuziki maarufu ambaye amepata tuzo ya Grammy ya muziki Yousou N'Dour, ambaye amezuiwa na mahakama kugombea kiti cha urais.

Rap-Sänger THIAT , Sprecher von der Bewegung Y'en a marre = bewegung der Zivilgesellschaft gegen die Kandidatur von Abdoulaye Wade 06-11.02.2012 in Senegal : in Dakar (Hauptstadt)

Mwimbaji wa mitindo ya Rap THIAT nchini Senegal,

Mwandishi : Sekione Kitojo / afpe

Mhariri: Bruce Amani

 • Tarehe 26.02.2012
 • Maneno muhimu Senegal
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/14AG8
 • Tarehe 26.02.2012
 • Maneno muhimu Senegal
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/14AG8

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com