Uchaguzi nchini Sierra Leone
13 Agosti 2007Matangazo
Huu ni uchaguzi wa kwanza kufanyika tangu wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa kuondoka miaka miwili iliyopita. Wapiga kura wengi walijitokeza kumchagua kiongozi wa taifa na wabunge. Rais Tejjan Kabah anamaliza kipindi chake cha uongozi baada ya kuwa madarakani tangu mwaka 2002 wakati vita vya wenyewe kwa wenyewe vilipokwisha. Vita hivyo vilidumu kwa miaka 11 na kuendelezwa na almasi. Ili kupata picha kamili Thelma Mwadzaya amezungumza na Said Msonga mkaazi wa Freetown, Sierra Leone.