1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

"Tunalinda Fedha za Umma wa Ujerumani"

10 Mei 2010

Umoja wa Ulaya na Shirika la Fedha la Kimataifa IMF zimeamua kuanzisha mfuko maalum wa Euro bilioni 750 katika jitahada ya kuzuia mzozo wa madeni ya serikali kuenea katika nchi za kanda inayotumia sarafu ya Euro.

https://p.dw.com/p/NKh6
German Chancellor Angela Merkel speaks during a news conference after a meeting of the party executive of the German Christian Democrats in Berlin, Germany, Monday, May 10, 2010. Voters ejected Chancellor Angela Merkel's center-right alliance from power in Germany's most populous state North Rhine-Westphalia on Sunday, costing the German leader her majority in the upper house of parliament and curb her government's power. Acknowledging a "bitter defeat" in a state election, German Chancellor Angela Merkel abandoned hopes Monday of pushing through tax cuts for Europe's biggest economy and said her government would concentrate on keeping Germany's debt down. (AP Photo/Michael Sohn)
Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel.Picha: AP

Viongozi wa Umoja wa Ulaya walijadiliana hadi asubuhi ya leo mjini Brussels, kabla ya kuidhinisha msaada huo wa dharura. Na Kansela wa Ujerumani, Angela Merkel na Waziri wa Mambo ya Nje Guido Westerwelle mjini Berlin hii leo walipaswa kuwaarifu wananchi kuhusu mpango huo mpya wa kuiokoa sarafu ya Euro. Safari hii, msaada huo hauhisiki na nchi yenye uchumi dhaifu katika kanda ya Euro, bali huo ni mpango wa kuitetea na kuilinda sarafu yao wenyewe. Mpango huo umeidhinishwa na Umoja wa Ulaya ili kukomesha ulanguzi unaoathiri thamani ya Euro katika masoko ya fedha duniani. Kansela Merkel amesema:

"Mpango huo utasaidia kuimarisha na kuilinda sarafu yetu. Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Euro na Umoja wa Ulaya, kuchukua hatua kama hiyo. Kwa maneno mengine, tunalinda fedha za umma wa Ujerumani."

Euro bilioni 500 zitachangwa na nchi za Umoja wa Ulaya na bilioni 250 zitatolewa na Shirika la Fedha la Kimataifa-IMF. Mpango huo umeidhinishwa na mawaziri wa fedha wa Umoja wa Ulaya, waliokutana kwa kikao cha dharura mjini Brussels siku ya Jumapili.

Bild 3. Westerwelle Porträt Titel: Guido Westerwelle Beschreibung Guido Westerwelle am Treffen des "Weimarer Dreiecks" in Bonn am 26./27. April 2010.
Waziri wa Mambo ya Nje wa Ujerumani, Guido Westerwelle.Picha: Marcin Antosiewicz

Lakini haitoshi tu kuwa tayari kutoa fedha hizo, amesisitiza waziri Guido Westerwelle.Yeye amesema, muhimu zaidi, ni kupiga vita chanzo cha mzozo huo wa Euro na kuongezea:

" Hiyo humaanisha kuwa kila nchi lazima ipunguze matumizi yake. Hata Ulaya ikubali kufanya marekebisho - yaani mfumo wa masoko ya fedha unapaswa kurekebishwa na hasa katika kuzuia ulanguzi."

Leo mchana, Kansela Merkel amewaalika katika ofisi yake wenyekiti wa vyama na viongozi wa vyama vinavyowakilishwa bungeni ili apate kuwaeleza zaidi kuhusu mpango huo mpya wa mabilioni ya Euro. Kiongozi wa wabunge wa chama cha upinzani cha SPD, Frank-Walter Steinmeier ameonyesha busara kuhusu hatua iliyochukuliwa. Amesema, chama chake hakikatai kuwa hatua ya kuleta utulivu katika kanda ya Euro imepaswa kuchukuliwa hata kwa usalama wa Ujerumani. Lakini matatizo hayo daima hayawezi kutenzuliwa kwa kuwapachika walipakodi gharama za mzigo huo kila wakati. Kwa hivyo ni matumaini yake kuwa serikali ya Ujerumani, sasa itachukua hatua za kurekebisha masoko ya fedha.

Hiyo kesho,baraza la mawaziri litashauriana kuhusu msaada huo wa mabilioni. Merkel amesema, uamuzi wa mswada wa sheria itakayoidhinisha mpango huo,sio lazima kuupitisha katika muda wa siku chache. Hata hivyo Merkel amesema, mpango huo unapaswa kuidhinishwa haraka na kikamilifu.

Mwandishi:Marx,Bettina/ZPR/P.Martin

Imepitiwa na: M-Abdul-Rahman