1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TSITELUBANI: Georgia na Urusi zalaumiana

8 Agosti 2007
https://p.dw.com/p/CBbD

Rais Mikhail Saakashvili wa Georgia ameilaumu Urusi kwa kujaribu kuzusha hofu kwa kutekeleza zoezi la ndege za kivita karibu na eneo lililojitenga la kusini mwa Ossetia.

Hata hivyo urusi imekanusha madai hayo na kusema kwamba ndege za kivita za Georgia ndizo zimehusika na kuangusha makombora hayo nchini mwake ili kuzusha hali ya wasiwasi katika eneo hilo.

Uhusiano kati ya nchi hizi mbili ni mbaya hasa baada ya Georgia kuwa na mipango ya kutaka kujiunga na muungano wa kijeshi wa magharibi NATO.