1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TRIPOLI:Mahakama kuu kutoa uamuzi juu ya wauguzi na daktari wakipalestina

11 Julai 2007
https://p.dw.com/p/CBk1

Taasisi ya Kadhafi nchini Libya imetangaza kupigwa hatua katika kesi inayowahusu wauguzi watano wakibulgaria na daktari mmoja wakipalestina waliokutikana na hatia mwaka 2004 ya kuwaambukiza makusudi virusi vya HIV watoto 438 wakilibya.

Taasisi hiyo imesema makubaliano juu ya kulipwa ridhaa yamefikiwa na familia za watoto hao.

Tangazo hilo limetolewa saa chache kabla ya mahakama kuu ya Libya kukutana hii leo kutoa hukumu yake iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu juu ya rufaa iliyokatwa na watuhumiwa hao.

Mwafaka.

Tangazo hilo limepokelewa kwa furaha na familia za wauguzi hao pamoja na daktari lakini familia za watoto hao ambao 56 miongoni mwao wameshakufa hazikupatikana kuzungumzia suala hilo.

Marekani ambayo imekuwa msitari wa mbele kuitolea mwito Libya kubadili msimamo wake juu ya kuwanyonga watu hao imepokea taarifa hiyo lakini kwa tahadhari.