Tieffensee akutana na wakuu wa GDL na Deutche Bahn | Habari za Ulimwengu | DW | 20.11.2007
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Tieffensee akutana na wakuu wa GDL na Deutche Bahn

,

Waziri wa uchukuzi wa Ujerumani Wolfgang Tieffensee amekutana na mkuu wa chama cha wafanyakazi madereva wa treni GDL Manfred Schell na mkuu wa shirika la reli la taifa Deutsche Bahnn Hartmut Mehdorn mjini Berlin .

Mazungumzo yao yalikuwa yamekusudia kuondowa kikwazo juu ya mzozo wao wa miezi kadhaa juu ya mishahara.Kufuatia mkutano huo Tiefensee amesema anatumai mazungumzo yataanza tena katikati ya wiki hii.GDL imekuwa ikigoma kuanza mazungumzo rasmi hadi hapo Deutsche Bahn itakapowasilisha pendekezo jipya juu ya madai yao ya nyongeza ya mishahara.

Schell na Mehdorn wanatazamiwa kuwa na mazungumzo leo hii. Chama cha wafanyakazi madereva wa treni kimefanya migomo kadhaa kudai ongezeko la mishahara la asimilia 31 kwa wanachama wake.

Ni muhimu kutuma kikosi Somalia

 • Tarehe 20.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CJVc
 • Tarehe 20.11.2007
 • Shirikisha wengine Tuma Facebook Google+
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CJVc

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com