1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEL AVIV: Waziri wa Mambo ya nchi za nje wa Marekani, Bibi Condoleeza Rice, ziarani mashariki ya kati.

13 Januari 2007
https://p.dw.com/p/CCau

Waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani, Bi Condoleeza Rice, amewasili nchini Israil kuanza ziara yake ya juma moja katika mashariki ya kati kwa lengo la kufufua mashauriano ya amani kati ya Israil na Wapalestina.

Bi Condoleeza Rice pia atazitembelea Misri, Jordan, Saudi Arabia na Kuwait.

Kweningeko Bi Condoleeza Rice amenukuliwa akisema kwamba agizo la hivi karibuni la kuwalenga wanamgambo wa Iran nchini Iraq, lilitolewa na Rais George W. Bush.

Bi Condoleeza Rice ameliarifu gazeti la New York Times kwamba uamuzi wa kukabiliana na mitandao ya Iran ni mojawapo wa mikakati ya kijeshi nchini Iraq.

Serikali ya Marekani inaishutumu Iran kwa kuwafadhili kifedha na pia kuwapa silaha wanamgambo wa kishia nchini humo.