1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN.Iran imo katika siku ya pili ya zoezi la kijeshi

3 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwO

Iran imesema kuwa imejaribu makombora yake matatu mapya katika siku yake ya pili ya zoezi la kijeshi katika ghuba ya Uajemi.

Kamanda wa kikosi cha jeshi la Iran amesema makombora hayo mapya yameimarishwa zaidi.

Watalaamu wa silaha wamesema kuwa makombora hayo matatu yana uwezo wa kushambulia kwa umbali wa hadi kilomita 2000 na hiyo ina maana kuwa makombora hayo yanaweza kuishambulia Israel au hata Ghuba ya Uajemi.

Wakati huo huo nchi tano wanachama wa baraza la usalama la umoja wa mataifa na Ujerumani zinajadili hatua ya kuiwekea vikwazo Iran kuhusu mpango wake wa nyuklia.

Urusi na China zimesha ashiria nia ya kupinga pendekezo la mswaada wa nchi za ulaya la kutaka Iran ifungiwe kuuziwa au kupelekewa malighafi au teknolojia itakayoiwezesha nchi hiyo kuendeleza na mpango wake wa nyuklia.

Mswaada huo pia utahusisha kuwekewa vikwazo vya usafiri na kutaifishwa kwa mali za watu wanaojihusisha na mpango wa nyuklia wa Tehran.

Naibu waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Kislyak amesema kuwa mswaada uliotayarishwa na Uingereza, Ufaransa na Ujerumani unahitaji kupigwa msasa.