1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Rais wa Iran asisitiza haki ya kuzalisha nishati ya nyuklia

11 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCTE

Rais Mahmoud Ahmedinejad wa Iran amekariri msimamo wa Tehran kuwa ina haki ya kuendeleza teknolojia ya kuzalisha nishati ya nyuklia. Ahmedinejad alitamka hayo alipohotubia umma mjini Teheran,kuadhimisha siku ya mapinduzi ya Kiislamu ya mwaka 1979 nchini humo.Akasisitiza kuwa Iran ina azma ya kutekeleza mradi huo kuambatana na mikataba ya kimataifa.Wakati huo huo akasema kuwa Iran ipo tayari kujadiliana na nchi za Magharibi kuhusu mradi wake wa nyuklia,lakini haitokubali dai la kusitisha kazi za kurutubisha madini ya Uranium.Nchi nyingi,zina hofu kuwa Iran kwa siri inajaribu kutengeneza silaha za nyuklia.Lakini serikali ya Tehran inashikilia kuwa mradi wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu.