1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN : Iran yataka mataifa magharibi yasitishe urutubishaji

20 Februari 2007
https://p.dw.com/p/CCQD

Katika mkesha wa kuamkia siku ya mwisho iliowekwa na Umoja wa Mataifa kwa Iran kusistisha urutubishaji wa uranium Iran imedokeza kwamba iko tayari kusistisha mpango wake wa kurutubisha uranium ili mradi mataifa ya magharibi nayo yanachukuwa hatua kama hiyo.

Rais Mahmoud Ahmedinejad amesema katika hotuba kaskazini mwa Iran kwamba hapo tena mazungumzo yanaweza kuanza chini ya mazingira ya haki.Amesema sio tatizo kwa nchi yake kusitisha urutubishaji wa uranium lakini mazungumzo yanayozingatia haki yanahitaji hatua kama hiyo kutoka mataifa ya magharibi.

Umoja wa Mataifa ulipiga kura kwa kauli moja kuunga mkono uwekaji wa vikwazo dhidi ya Iran baada ya nchi hiyo kupuuza madai ya chombo hicho yaliotolewa huko nyuma kuitaka isitishe urutubishaji huo.

Iran inakabiliwa na uwezekano wa kuwekewa vikwazo zaidi venginevyo inasitisha urutubishaji huo ifakapo hapo kesho ikiwa ni mwisho wa siku 60 ilizopewa na Umoja wa Mataifa kufanya hivyo.