1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TEHRAN: Iran yataka kuachiliwa raia wake wanaoshikiliwa na Marekani nchini Iraq.

Iran imetoa wito wa kuachiliwa mara moja raia wake watano waliokamtwa na majeshi ya Marekani nchini Iraq.

Iran pia imekanusha madai yaliyotolewa kwamba raia hao ni majasusi waliopelekwa kuwasaidia wanamgambo nchini humo.

Watu hao watano walikamatwa alhamisi iliyopita katika mji wa Arbil kaskazini mwa Iraq.

Majeshi ya Marekani yamedai kuwa watu hao ni askari-jeshi waliokuwa wakiwapa silaha wanamgambo, madai ambayo Iran imeyakanusha ikisema watu hao walikuwa maafisa wa kibalozi.

Hivi karibuni Marekani ilitahadharisha kwamba itakabiliana vikali na raia wa Iran wanaowasaidia wanamgambo wa kishia nchini Iraq.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com