1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Iran yasema haitakutana na Marekani

1 Mei 2007
https://p.dw.com/p/CC5U

Iran imefutilia mbali uwezekano wa kufanya mazungumzo na waziri wa mashauri ya kigeni wa Marekani, Condoleezza Rice, kwenye mkutano wa kilele kuhusu usalama wa Irak utakaofanyika katika mji wa mapumziko wa Sharm el Sheikh nchini Misri.

Waziri wa mashauri ya kigeni wa Iran, Manouchehr Mottaki, atahudhuria mkutano huo pamoja na waziri Condoleezza Rice, hivyo kuzusha matumaini ya uwezekano wa viongozi hao wawili kufanya mazungumzo baina ya Iran na Marekani kwa mara ya kwanza tangu mwaka wa 1980.

Hapo awali Iran ilisita kushiriki kwenye mkutano huo wa Sharm el Sheikh utakaoanza Alhamisi na kumalizika Ijumaa wiki hii, ikisema haikufurahishwa na hatua ya Marekani kushiriki kwenye mkutano huo pamoja na mataifa jirani na Irak.

Lakini uamuzi wake kumtuma waziri wa mashauri ya kigeni Mottaki kuhuhduria kikao hicho kulizusha tatesi kwamba waziri huyo angefanya mazungumzo ya kihistoria na Condoleezza Rice. Marekani ilikataa kufutilia mbali uwezekano huo.