1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHRAN: Ahmadinejad ayataka mataifa ya magharibi yawe rafiki wa Irak

11 Oktoba 2006
https://p.dw.com/p/CD3q

Rais wa Iran Mahmoud Ahmadinejad ameyataka mataifa ya magharibi yawache kuikasirikia nchi yake.

Kiongozi huyo ametaka badala yake nchi za magharibi ziwe marafiki na Iran, ambayo amesema inaendelea kuwa na nguvu huku mataifa hayo yakiendelea kupoteza nguvu na uwezo wao.

Katika hotuba yake mjini Shahriar, nje ya mji mkuu Tehran, rais Ahmadinejad ameuliza ni faidi gani waliyopata viongozi wa mataifa ya magharibi katika miaka 27 ya kuikasirikia na kuichukia Iran.

Rais Ahmadinejad ameyasema hayo wakati baraza la usalama la Umoja wa Mataifa likijadili uwezekano wa kuiwekea vikwazo Iran kuhusiana na mpango wake wa kinyuklia.