1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

TEHERAN: Mazoezi ya kijeshi ya Iran yameanza Ghuba ya Uajemi

2 Novemba 2006
https://p.dw.com/p/CCwk

Iran imeanzisha mazoezi ya kijeshi ya siku kumi kwa kurusha makombora yenye uwezo wa kubeba mabomu ya kinuklia.Wataalamu wanasema makombora ya Iran aina ya Shahab-3 yana uwezo wa kwenda umbali wa hadi kilomita 2,000 na kufika hadi Israel na hata kwenye vituo vya kijeshi vya Kimarekani katika Ghuba ya Uajemi.Kamanda wa majeshi ya Iran alikiambia kituo cha televisheni cha Al-Alam,makombora darzeni kadhaa yatarushwa wakati wa mazoezi,kuonyesha nguvu za taifa hilo kujitetea kijeshi.Tangazo hilo limetolewa siku mbili baada ya manowari za kijeshi za Marekani kukamilisha mazoezi ya siku mbili katika Ghuba ya Uajemi.