TBILISI: Mzozo kati ya Georgia na Urusi unazidi | Habari za Ulimwengu | DW | 02.10.2006
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

TBILISI: Mzozo kati ya Georgia na Urusi unazidi

Hali ya wasiwasi inazidi kati ya Urusi na nchi jirani ya Georgia. Rais wa Uursi Vladamir Putin amekosoa vikali kutiwa mbaroni kwa maofisa wanne wa jeshi la Urusi na maofisa wa usalama wa Georgia kwa kuwa makachero.

Katika matamshi yake yaliyotangazwa katika runinga ya kitaifa baada ya kukutana na baraza lake la usalama, rais Putin amekieleza kitendo cha kukamatwa kwa wanajeshi hao kuwa ugaidi wa kitaifa ulioambatana na utekaji nyara.

Ameulinganisha utawala wa Georgia kama Lavrenty Beria, ambaye kama kiongozi wa polisi ya muungano wa Soviet, aliongoza juhudi za safisha safisha za rais Stalin katika miaka ya 1930 na 1940 zilizosababisha vifo vya mamilioni ya warusi.

Wakati huo huo, Urusi imeowaondoa maofisa wake wote katika ubalozi wake mjini Tbilisi na kusimamisha makubaliano ya kuwaondoa wanajeshi wake kutoka Georgia yaliyoafikiwa hapo awali.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com