1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Tallinn. Estonia. Waandamanaji wafanya uporaji na ghasia.

27 Aprili 2007
https://p.dw.com/p/CC6V

Mtu mmoja ameuwawa na wengine 43 wamejeruhiwa katikati ya mji wa Tallinn , katika tukio la uporaji maji usiku na mapambano na polisi. Uharibifu na uporaji ulizuka katika mji mkuu wa Estonia jana Alhamis wakati polisi walipowalazimisha waandamanaji kutawanyika kutoka katika eneo la kumbukumbu ya vita la Urusi ya zamani.

Zaidi ya watu 300 walikamatwa kufuatia ghasia hizo. Baada ya kikao cha dharura , serikali ya Estionia ililiondosha sanamu la askari wa jeshi la Urusi mapema leo asubuhi.

Russia imesema kuwa imekasirishwa na hatua hiyo na baraza lake la Seneti limepiga kura kumtaka rais Vladimir Putin kuvunja uhusiano na nchi hiyo ndogo katika eneo la Baltic. Ghasia hizo zilikuwa mbaya kuwahi kuonekana tangu Estonia kupata uhuru kutoka Russia mwaka 1991.