Taarifa za michezo wiki hii | Michezo | DW | 10.11.2006
 1. Inhalt
 2. Navigation
 3. Weitere Inhalte
 4. Metanavigation
 5. Suche
 6. Choose from 30 Languages

Michezo

Taarifa za michezo wiki hii

Miongoni mwazo ni Bayern Munich kuchuana na Bayer Leverkusen Jumamosi hii . Jee baada ya kufungwa nyumbani na Hannover katikati mwa wiki itamudu kutamba ugenini.

Ligi kuu ya Ujerumani Bundsliga Jumamosi hii inatimua tena vumbi, huku Bayern Munich ikiwania kujisogeza katika msimamo jumla baada ya katikati ya juma kujikuta ikishuka hadi nafasi ya tano, ilipofungwa kwa mshangao na Hannover tena nyumbani Munich bao moja kwa bila. Matokeo hayo yaliiacha Werder Bremen ikiongoza kwa tafauti ya pointi 6 na Bayern Munich. Na pia kutoa changa moto kwa mabingwa hao watetezi .

Bayern Itaumana na Bayer Leverkusen mjini Leverkusen mchezo ambao ni mgumu kutabiri. Katika mechji nyengine jioni hii Schalke nao wako Mainz, huku Wolfsburg wakichuana na Cottbus,Hamburg inaikaribisha Borussia Monchengladbach na frankfurt inaumana na Arminia Bielefeld. Stuttgart ilioko nafasi ya pili itakua uwanjani kesho mjini Hannover ikiuamana na Hannover 96.

Wakati huo huo bayer Leverkusen inapanga kuwa na kocha Michael Skibe kwa muda mrefu licha ya matokeo yasio mazuri kama ilivyotegemea hadi sasa katika msimu huu kwenye michuano yake ya ligi.

Mkuu wa kilabu hiyo Wolfgang Holzhaeuser alisema kwamba wanapanga kurefusha mkataba wa Skibe utakaomalizika mwishoni mwa msimu huu. Skibe alikua msaidizi wa Rudi Voeller alipokua Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani kwa miaka 4 hadi yalipomalizika mashindano ya kombe la Ulaya 2004. Tangu Oktoba mwaka jana amejiunga na Leverkusen baada ya Klaus Augenthaler kuihama kilabu hiyo.

Leverkusen iko nafasi ya 9 katika msimamo wa ligi kuu na wameshatolewa katika kombe la Ujerumani, walipofungwa na timu ya daraja la pili MSV Duisburg. Shirikisho la vyama vya kandanda barani Ulaya UEFA, limemfungia mechi mbili za kimataifa mchezaji wa Werder Bremen ya Ujerumani Aron Hunt kwa tabia inayokwenda kinyume na michezo.

Kufungiwa mshambuliaji huyo kunatokana ana matamshi ya kibaguzi aliyowatolea wachezaji wa Uingereza katika pambano la kimataifa la wachezaji chini ya umri wa miaka 21 mjini Leverkusen mwezi uliopita.

Chama cha soka cha England kililalamika kwamba wachezaji wenye asili ya kiafrika wa timu ya England Micah Richards na Anton Ferdinand waliitwa „kima“ na Hunt baada ya England kuilaza Ujerumani mabao 2-0. Hunt ambaye mama yake ni Muingereza na baba Mjerumani amekana madai hayo.

Miamba ya kandanda nchini Ureno kilabu ya Benfica ya mjini Lisbon, wameweka rekodi mpya kwa kuwa na wanachama wengi zaidi wenye kutoa michango yao na kuipiku kilabu maarufu ya Uingereza Manchester United. Gazeti la michezo mjini Lisbon linalotoka kila siku A Bola lilisema jana kwamba Benfica ilioanzishwa 1904 sasa ina wanachama 160,000 ikilinganishwa na 152,000 wa Manchester United ambayo hapo kabla ndiyo iliokua ikishikilia rekodi hiyo.

Msimu uliopita Benfica ilijingia Euro milioni 13 kutokana na malipo ya wanachama na idadi hiyo ilikua ni asili mia 14 ya mapato yake jumla. Benfica iko katika kundi moja la F na Manchester United katika michuano ya kuwania kombe la ubingwa wa ulaya-Champions league- ikiwa nafasi ya tatu. Manchester inaongoza kundi hilo ikifuatwa na Celtic ya Scotland.

Wakati Afrika kusini ikijandaa kuwa mwenyeji wa kombe lijalo la dunia 2010, makampuni kutoka mkoa wa kusini mwa Ujerumani wa Bavaria yatakua washauri wa maafisa wa maandalizi wa Afrika kusini katika masuala ya usalama, afya na masuala ya vyombo vya habari .

Katibu mkuu wa Waziri mkuu wa jimbo la Bavaria Edmund Stoiber ametoa taarifa wiki hii akithibitisha kwamba mkoa wake utachangia wataalamu katika masuala yote hayo. Ujerumani ndiyo iliokua muandalizi wa mashindano yaliopita ya kombe la dunia mwaka 2005 na mji mkuu wa Bavaria-Munich ulikua mwenyeji wa sherehe za ufunguzi na mechi ya

 • Tarehe 10.11.2006
 • Mwandishi Mohammed AbdulRahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcy
 • Tarehe 10.11.2006
 • Mwandishi Mohammed AbdulRahman
 • Chapisha Chapisha ukurasa huu
 • Kiungo http://p.dw.com/p/CHcy