1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Syria yaimarisha nguvu za wanajeshi wake katika mlima wa Golan

Oummilkheir22 Februari 2007

Hofu zimezidi pasije pakazuka vita kati ya Israel na Syria

https://p.dw.com/p/CHJW
Eneo la Golan
Eneo la GolanPicha: AP

Ripoti za kuimarishwa,kwa msaada wa Iran,shughuli za wanajeshi wa Syria katika milima ya Golan inayokaliwa tangu mwaka 1967 na Israel,zinapalilia uvumi wa kuripuka vita pamoja na Israel.

Jeshi la Syria hivi karibuni limekua likiamuru wanajeshi wake kuelekea katika mpaka na Israel,katika mlima wa Golan-hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya gazeti la Haaretz iliyotangazwa hii leo.

Ripoti hiyo iliyoandikwa na mtaalam maaruf wa gazeti la Haaretz kuhusu masuala ya ulinzi,ZEEV Schiff,inahoji Syria imejibagwa katika mbio za kujirundikia silaha kwa msaada wa Iran-adui mkubwa wa Israel.

Ripoti hizo zinafuatia taarifa za hivi karibuni za afisa wa idara ya upelelezi wa kijeshi ya Israel,jenerali Yossi BEIDATZ aliyedai tunanukuu: rais Bachar el Assad wa Syria anawaandaa wanajeshi wake kuweza kukabailiana kijeshi na Israel”.

“Mzozo huo unaweza kuchochewa na mtu mwengine” ameashiria wiki hii jenerali huyo,akimaanisha Hisbollah ambao Israel ilipambana nao kwa zaidi ya mwezi mmoja msimu wa kiangazi uliopita-bila ya kuibuka na ushindi.

“Jeshi la Syria limekua tangu siku za hivi karibuni likijiimarisha kwa kasi na kila upande,kutokana na msaada wa fedha wa Iran-ameandika Zeev Schiff,ambae ni ripota wa masuala ya kijeshi wa gazeti la Haaretz.

“Katika mbio hizi za kujirundukia silaha-kipa umbele ni makombora ya masafa marefu”-anaandika ripota huyo .

Kwa maoni yake Syria imejikusanyia makombora chapa SCUD-D yanayoweza kushambulia hadi umbali wa kilomita 400-kuweza kulenga sehemu kubwa ya ardhi ya Israel.Zeev Schiff anashadidia hoja zake kwa kusema Syria imeyajarivbu kwa ufanisi makombora hayo hivi karibuni ,kuweza kufidia jeshi la anga ambalo ni dhaifu.

Gazeti la Haaretz limeongeza kuandika kwamba serklai ya Damascus imetiliana saini “makubaliano ya aina pekee” pamoja na Urusi,kuhusu kupatiwa makombora elfu kadhaa yenye uwezo wa kushambulia vifaru vya kimambo leo, yaliyotumiwa na Hisbollah dhidi ya Israel msimu wa kiangazi uliopita.

“Vikosi vya Syria vinaranda randa vikielekea karibu na mpakani katika milima ya Golan” ameendelea kuandika Zeev Schiff akikumbusha nyendo kama hizo ndizo zilizopelekea kuripuka mashambulio ya Syria katika uwanja huo wakati wa vita vya Kipour kati ya Israel na waarabu mnamo mwaka 1973.

Hata hivyo jenerali wa akiba wa Israel,Amos Gilad,mshauri wa waziri wa ulinzi Amir Peretz amesema kupitia Radio Israel,”hawana habari zozote zinazoonyesha kwamba Syria inajiandaa kuihujumu Israel miezi ijayo.”

“Kwamba Syria inaimarisha nguvu zake za kijeshi haimaanishi kwamba watatushambulia,japo kama tunabidi kweli kujiandaa-ameongeza kusema jenerali Amos Gilad,aliyungama kwamba ripoti za Schiff mara nyingi ni za kuaminika.

Hakukanusha lakini na wala hakudhibitisha kuhusu piripa pirika za wanajesshi wa Syria katika eneo la mpakani,katika mlima wa Golan.

Wakati huo huo jeshi la Israel lnaripotiwa kufanya luteka kubwa hapo jana katika eneo hilo la Golan,vikishiriki vikosi vya nchi kavu,vifaru na jeshi la wanaanga.

Waziri wa ulinzi Amir Peretz aliyeshuhudia luteka hizo amesema “hazimaanishi kwamba wanajiandaa kwa vita vya aina yoyote ile.