SUFFOLK:Bata mzinga laki moja na alfu 60 waangamizwa nchini Uingereza | Habari za Ulimwengu | DW | 05.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SUFFOLK:Bata mzinga laki moja na alfu 60 waangamizwa nchini Uingereza

Zoezi la kuangamiza bata zaidi ya laki moja na alfu 60 limeendelea nchini Uingereza kwa lengo la kuzuia kuenea ugonjwa wa homa ya ndege. Zoezi hilo lilianza jana kwenye shamba kubwa katika mji wa Suffolk mashariki mwa Uingereza. Wanasayansi wanahofia kuwa aina kali ya ugonjwa huo iliyoua watu zaidi ya 160 katika nchi mbalimbali inaweza kugeuka na kusababisha maambukizi baina ya binadamu kwa urahisi na kwamba mamilioni ya watu wanaweza kufa duniani kote.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com