1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

St. PETERSBURG : Polisi yapambana na wapinzani wa serikali

4 Machi 2007
https://p.dw.com/p/CCMb

Madarzeni ya watu wamekamatwa baada ya polisi ya Urusi kuvunja maandamano ya upinzani katika mji wa St.Petersburg.

Miongoni mwa waliotiwa mbaroni ni watayarishaji kadhaa wa maandamano hayo.Polisi wakiwa na zana za kuzima ghasia walipambana na waandamanaji baada ya kuvunja vizuizi vya polisi. Zaidi ya watu 3,000 imeripotiwa kuwa wameshiriki maandamano hayo ambayo yameitishwa kuipinga serikali ya Rais Vladimir Putin.

Maandamano hayo yalikuwa hayakupata kibali cha serikali.