Siku ya kufunguliwa misikiti Ujerumani
Kiasi ya misikiti 1,000 inafunguliwa milango yake kwa ajili ya wageni siku ya Oktoba 3 ya kila mwaka chini ya kaulimbiu "Jamii nzuri, Jamii salama". " DW inaangazia tukio hili katika nyumba za ibada za Kiislamu.
Misikiti ya Ujerumani- Umoja wa Ujerumani
Siku ya "kufunguliwa misikiti" imeanza tangu mwaka 1997 sambamba na siku ya Muungano wa Ujerumani, ambayo ni siku ya mapumziko Kitaifa. Siku hiyo ilichaguliwa kuelezea mahusiano kati ya Waislamu na Wajerumani na namna wanavyojichukulia kama sehemu ya muungano huo, linaeleza baraza kuu la Waislamu. Kiasi ya wageni 100,000 hutarajiwa, baadhi yao wamesimama mbele ya msikiti wa Sehitlik, mjini Berlin.
Misikiti kwa wote
Katika siku hii, jamii ya Kiislamu inataka kuwaelewesha Wageni kuhusu Uislamu, Zaidi ya eneo la ibada, misikiti pia hutumika kama eneo la kukutana ili kujenga umoja na kubadilishana mawazo. Jina "msikiti" limetokana na neno la Kiarabu "masjid" linalomaanisha "eneo la kusujudu kwa sala".
Taratibu na sheria
Sehemu ya kuujua Uislamu ni kuzijua kwanza sheria na taratibu zake. Utaratibu wa awali ni kuvua viatu kabla ya kuingia kwenye chumba cha ibada. Kinachozingatiwa ni usafi na utakaso: kabla ya kila sala, Waislamu hufanya udhu. Kwa kuwa waumini hugusa zuria la ibada na paji la uso, hivyo mazuria hayo wakati wote hutakiwa kuwa masafi.
Usanifu na historia
Misikiti mingi hutoa watu watakaoongoza wageni, kama inavyoonekana hapo juu kwenye msikiti huu ulioko Hürth, karibu na Cologne. Hapa, wageni wanaweza kupata picha ya usanifu wa Kiislamu, historia na maisha ya kila siku kwenye misikiti, ili kufahamu zaidi kuhusu namna jamii ya Kiislamu nchini Ujerumani inavyokusanyika kujenga umoja.
Kushirikishana kwenye Ibada
Msikiti wa Merkez ulioko Duisburg, uliofunguliwa mwaka 2008, ni mkubwa zaidi nchini Ujerumani. Shughuli zinazohusiana na mahusiano ni miongoni mwa zinazotiliwa umuhimu kwa jamii ya Kiislamu ya Duisburg. Kwa pamoja na wanaoongoza wageni kwenye msikiti huo, wageni pia hupata nafasi ya kuhudhuria ibada za adhuhuri na alasiri. Baadaye, wageni hukaribishwa kupata kikombe cha chai.
Kushirikishana sala
Kuijua ibada ya Kiislamu ni moja ya masuala muhimu kwenye tukio hili la Oktoba 3. Lakini wageni hawaruhusiwi kufikia maeneo halisi ya sala. Kama inavyoonekana katika msikiti huu wa Sehitlik, wageni wanasikiliza sala kutokea eneo hili la kusimama lililopo juu. Neno sala, kwa kiarabu ni "salah" ama "salat," ambayo kimsingi inamaanisha "mahusiano na Mungu."
Misbaha na rozali
Kijana huyu alipewa cheni yenye shanga za sala katika siku hiyo ya kufunguliwa misikiti huko Frankfurt. Waumini husukuma shanga na vidole vyao na kurudia sala na kughani, kama inavyofanywa na Wakristu na Wabuddha. Cheni hii, yenye angalau shanga 33, inaitwa "tasbih" ama "misbaha" katika Uislamu. Shanga hizo zimedhihirisha umuhimu wake wakati wanaporudia majina 99 ya Allah.
Mjadiliano ya tamaduni tofauti
Misikiti nchini Ujerumani hufungua milango ili kuwaelimisha watu kuhusu jadi hata kupitia matukio mengine. Kwa mfano, wakati wa mkutano wa Wakristo nchini Ujerumani, Wakatoliki, watawa huwaongoza wageni, kama wanavyoonekana hapa katika msikiti wa Yavuz Sultan Selim ulioko Mannheim. Matukio kama hayo hutoa nafasi kwa Wakristu na Waislamu kuimarisha mahusiano na kuwa ya karibu zaidi.
Kuvunjwa kwa chuki zisizo na msingi
Msikiti uliopo Dresden hualika wageni kutambulishana tamaduni pia. Msikiti wa Al-Mostafa umekwishatangaza ratiba ya matukio: kutakuwa na mihadhara itakayoongozwa na imam kuhusu Uislamu, Mtume Muhammad na Koran, na muda wa mazungumzo pamoja na viburudisho, kujifunza na kujadili. Katika mji ambako kundi linalopinga Uislamu la PEGIDA liligonga vichwa vya habari, tukio kama hili lina umuhimu mkubwa.