1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

131211 Welthungerhilfe Jubiläum

Sekione Kitojo14 Desemba 2011

Leo (14.12.2011) Shirika la Kupambana na Njaa Duniani linatimiza miaka 50 tangu kuundwa kwake, ambalo linaadhimisha siku hii kwa matukio mbalimbali, ikiwa ni pamoja na mauzo kwa mnada na kampeni za msaada.

https://p.dw.com/p/13SKm
Foleni ya kusubiri chakula nchini Bangladesh
Foleni ya kusubiri chakula nchini BangladeshPicha: picture-alliance/dpa

Shirika hili, Welthungerhilfe, lililoanzishwa tarehe 14 Disemba 1962 chini ya mwavuli wa Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), hivi sasa ndilo shirika kubwa kabisa la binafsi linalotoa misaada katika Ujerumani. Hata katika miaka hiyo 50 ya kuwapo kwake, shirika hilo limehakikisha kuendelea kuwapatia chakula watu pamoja na maendeleo ya nchi na lina uwezo na mali ya kuweza kufanya kazi hiyo.

Kwa ujumla katika muda wa miaka hii 50, shirika hilo limekuwa likijishughulisha na miradi 4,500 ya kujisaidia wenyewe na miradi 1,100 kwa ajili ya watoto na vijana katika nchi karibu 70 duniani. Pamoja na hayo kuna mipango karibu ya 1,000 ya msaada wa dharura.

"Muhimu sana katika miaka hii 50, ni kwamba suala la msingi katika lengo letu, ni kuwakomboa watu kutokana na njaa, kwa kutoa misaada ya kujisaidia wenyewe na kuwapa fursa ya kuweza kuishi, bila ya njaa, na kujiendeleza." Amesema Bärbel Diekmann, rais wa shirika hilo na meya wa muda mrefu wa jiji la Bonn, akielezea kazi za shirika hilo kwa jumla katika miongo iliyopita.

Mfano wa mafanikio kwa shirika hili la Welthungerhilfe ni kupiga hatua kwa nchi kama Chile, Thailand na Angola, baada ya hali ya kijamii na kiuchumi katika nchi hizo kuwa bora.

Mamilioni ya watu wamepata msaada kupitia shirika hili la Welthungerhilfe katika miongo iliyopita kwa kuweza kupata misaada. "Mwaka 1969 asilimia 26 ya watu duniani walikuwa wana utapia mlo, mwaka 2010 idadi hiyo ilikuwa ni asilimia 13.

Mkuu wa Welthungerhilfe, Bärbel Dieckmann
Mkuu wa Welthungerhilfe, Bärbel DieckmannPicha: picture-alliance/dpa

Hii ina maana, kwa hakika matokeo hayo mara nyingine ambayo hayawezi kutabirika, yanasababishwa na ukuaji mkubwa wa idadi ya watu. Sehemu ya asilimia ya watu wanaokabiliwa na njaa na jumla ya watu wote duniani imeongezeka katika miaka ya hivi karibuni. Na haya si mafanikio pekee ya shirika hili la msaada wa chakula." Anasema Diekmann.

Kwa upande mwingine watu zaidi ya milioni 930 duniani wanasumbuliwa bado na njaa na umasikini. Hili haliwezi kukubalika, anasema rais wa Welthungerhilfe.

Kutokana na hilo mambo mbali mbali ya kilimwengu kama mabadiliko ya tabia nchi, upungufu wa maliasili na hali ya ongezeko la idadi ya watu, yanaifanya mada ya maendeleo kutotiliwa maanani katika majadiliano, na kwamba suala sasa ni kile kinachoelezwa kuwa nchi zinazoinukia kiuchumi, ameeleza rais wa Welthungerhilfe. Ndio sababu anataka shirika hilo kuliimarisha katika mwaka ujao kwa kujiingiza zaidi katika jamii, katika mapambano dhidi ya njaa.

Mjadala ambao kwa muda wa miaka 50 haukufanyika ni kuhusu uwezo. Diekmann anasema kuwa ukosefu wa nishati ni sababu kuu inayosababisha umasikini na njaa. Na haya ni matatizo kwa mtazamo wake ambayo yanazidi kuwa mabaya.

Katika nchi nyingi ambazo tunafanyakazi, upatikanaji wa nishati ni msingi wa maendeleo ya watu hasa vijijini. Ni pale tu itakapopatikana nishati ya kutosha ndipo tutaweza kumshinda adui njaa hapo baadaye.

Mwandishi: Sabine Rippberger
Tafsiri: Sekione Kitojo
Mhariri: Josephat Charo