1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sheria za upelelezi ziondolewe vizingiti

P.Martin29 Julai 2007

Rais wa Marekani,George W.Bush ametoa wito kwa Bunge kuregeza vikwazo vinavyohusika na upelelezi wa washukiwa ugaidi.

https://p.dw.com/p/CHAN

Katika hotuba yake ya kila juma kwenye redio,Bush aliwahimiza wabunge waidhinishe sheria ya FISA ya mwaka 1978 inayohusika na utaratibu wa upelelezi ambayo imefanyiwa marekebisho kulingana na hali ya sasa.

Bush amesema,magaidi wanatumia teknolojia ya kisasa kama vile simu za mkono na mtandao wa Internet.Akaongezea kuwa teknolojia ya aina hiyo haikuwepo pale sheria ya FISA ilipopitishwa takriban miaka 30 iliyopita na haikufanyiwa mageuzi kuambatana na maendeleo ya kiteknolojia.Kwa hivyo,taifa linazuiliwa katika uwezo wake wa kupata habari za upelelezi zinazohitajiwa,ili kuweza kuhifadhi usalama wa umma.

Mswada wa sheria uliopendekezwa na Ikulu ya Washington katika mwezi wa Aprili,unataka kuregeza vikwazo kuhusika na udakaji wa barua pepe,mazungumzo ya simu na mawasiliano mengine nchini Marekani.

Wabunge wa chama cha Demokratik wamesema,wao hawatoidhinisha marekebisho hayo.