1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sherehe za tamasha la muziki wa Bayreuth kuanza Jumapili

Sekione Kitojo23 Julai 2010

Pazia litafunguliwa mwishoni mwa juma hili katika tamasha la muziki la Bayreuth hapa Ujerumani, ambalo linatarajiwa kufunguliwa rasmi kwa muziki mpya wa opera wa Richard Wagner.

https://p.dw.com/p/OTMq
Kiongozi wa muda mrefu wa tamasha la muziki la Bayreuther Festspiele, Wolfgang Wagner, akiwa mbele ya jengo la ukumbi wa Bayreuth , wa Festspielhaus.Picha: picture-alliance/dpa

Pazia  litafunguliwa   mwishoni  mwa  juma  hili  katika tamasha  la  kale  nchini  Ujerumani   la  Bayreuth, ambalo linatarajiwa  kufunguliwa  rasmi  kwa  muziki  mpya  wa opera   wa  Richard  Wagner  unaofahamika  kama Lohengrin.

Julai 25  , siku  ya  Jumapili  linaanza  tamasha  la  99  la Bayreuther, tamasha  la  kila  mwaka  majira  haya  ya kiangazi. tamasha  la  muziki  ambalo  linalenga  tu   katika kazi  za  Wagner  na  litakuwa  la  kwanza   tangu  kifo  cha mjukuu  wa  mtunzi  huyo  maarufu  ambaye  alikuwa mkuu  wa  zamani  wa  tamasha  hilo, Wolfgang  Wagner, mapema  mwaka  huu.

Kuchezwa  kwa  muziki  huo  mpya   unaojuliakana  kama Lohengrin  kunakosubiriwa  kwa   shauku  kubwa , kunakotarajiwa  kufanywa  na  muongozaji   maarufu nchini  Ujerumani  Hans  Neuenfels, mwenye  umri  wa miaka  69,  ni  tayarisho  jipya   ambalo  litaonyeshwa katika  ukumbi  wa  Festspiehaus  mjini  Bayreuth  katika muda  wa  miaka  miwili.

Tamasha  la  mwaka  jana    lilikuwa  tu  la  kumbukumbu ya   ngano  za  zamani   katika  muziki   na  kuruhusu mabadiliko  ya  uongozi  katika  ngazi  ya  juu  kwa  njia isiyo  na  utata. Wagner  ambaye  alitawala  katika  vilima vya  Green  Hill   huko   Bayreuth  kwa  mkono  wa  chuma kwa  miaka  57  alikabidhi  u  hatamu  za  uongozi  kwa wanawe  wa  kike, Eva  Wagner-Pasquier, mwenye  umri wa  miaka  65  na  Katharina Wagner  mwenye  umri  wa miaka  32.

Kwa  hiyo , Lohengrin , utakuwa  utayarishaji  mpya  wa kwanza   chini   ya  uongozi  mpya  wa  pamoja kama anavyoelezea  Christian  Thielemann  ambaye  ni   mmoja wa  waongozaji  katika  tamasha  la  Bareuth.

Tunaangalia  kwa  undani  muziki  huu  wa  Wagner, na hatuwezi  kusahau, watu  wa  kwaya  na  wanamuziki  kuwa wanakuja  hapa  kwa  ajili  ya  mapumziko  yao. Pia wanajumuika  katika  kupiga  muziki  kwa  mapenzi  yao. Yule  anayekuja  hapa, anataka  kuja. Na  hili  ndio muhimu  sana. Hakuna  utaratibu  wa  kazi. Hapa  tunapiga muziki, yule  asiyetaka, halazimiki  kuja  hapa.

Kwa  kuwa  na  nyota  wa  sauti  ya  tatu  nyembamba kutoka  hapa  Ujerumani  Jonas Kaufmann  akiwa  ndio kwanza  anajitokeza  katika  tamasha  hili  la  mjini Bayreuth , akiwa  anachukua  nafasi  ya  juu, pamoja  na kijana  anayekuja  juu  pia   ambaye  ni  muongozaji kutoka  Latvia  Andris Nelsons , matarajio  yako  juu  sana kuliko  kawaida.

Bayreuth  ni   moja  kati  ya  maeneo  muhimu  sana katika  matamasha  ya  muziki  wa  opera  pamoja  na muziki  laini, ambapo  watu  hutoa  maombi  ya  kuingia katika  tamasha  hilo, ikiwa  orodha  inafika  hadi  miaka kumi. Tamasha  hilo  huanza  kwa  kawaida  Julai  25  hadi August  28  na  siku  ya  ufunguzi  huhudhuriwa  kwa kawaida  na  Wajerumani  ambao  ni  maarufu  kijamii  na kisiasa.

Mwandishi : Sekione  Kitojo / AFPE

Mhariri : Mohammed  Abdul-Rahman