SHARM EL SHEIKH:Iran yaishambulia Marekani na kusema isimtafute mchawi wa matatizo ya Iraq | Habari za Ulimwengu | DW | 04.05.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

SHARM EL SHEIKH:Iran yaishambulia Marekani na kusema isimtafute mchawi wa matatizo ya Iraq

Iran imetupa makombora makali dhidi ya siasa za Marekani nchini Iraq na kusema kuwa kuwepo kwake huko ndiko chanzo cha umwagikaji mkubwa wa damu.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran Manouchehr Moattaki akizungumza katika mkutano wa kimataifa juu ya Irak nchini Misri amesema Marekani ni lazima ikubali kuwa kuongezeka kwa maasi nchini Iraq, ni kutokana na kuwepo kwao huko na wasitafute mchawi.

Mapema ilielezwa kuwa Waziri huyo wa nje wa Iran ilikuwa akutane hii leo pembezoni mwa mkutano huo, na waziri wa nje wa Marekani Condoleza Rice.Hata hivyo bi Rice amesema kuwa bado hawajatana.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com