Shanghai: Bei za hisa za makampuni duniani zimepanda kidogo baada ya mshtuko wa jana | Habari za Ulimwengu | DW | 28.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Shanghai: Bei za hisa za makampuni duniani zimepanda kidogo baada ya mshtuko wa jana

Bei za hisa za makampuni katika Uchina leo ziliuzwa kwa bei ya juu zaidi ukilinganisha na jana pale ziliposhuka kwa ghafla, hivyo kusababisha hali kama hiyo duniani kote. Soko la Shanghai lilipata nguvu leo, hisa zake zikipanda bei kwa asilimia 3.94 baada ya jana kuwa na hasara kubwa kabisa isiowahi kuonekana mnamo mwongo mmoja uliopita. Mporomoko huo ulifanya soko la hisa la hapa Ujerumani, Dax, kupoteza bei kwa zaidi ya asilimia mbili lilipofungwa jana jioni. Pia lile la New York la Dow Jones lilipoteza bei kukiweko wasiwasi kwamba bei za hisa katika Marekani na China ni ghali. Leo masoko mengine ya hisa duniani hayajafanya biashara kubwa.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com