1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Ujerumani yajadili kubana matumizi

Sekione Kitojo7 Juni 2010

Serikali ya Ujerumani jana Jumapili ilianza kikao cha siku mbili cha baraza la mawaziri ili kujadili juu ya kubana matumizi kutokana na nakisi kubwa katika bajeti ya serikali.

https://p.dw.com/p/Njro
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel anamatumaini kuwa uamuzi utakaofikiwa katika kikao cha baraza la mawaziri utaleta mafanikio kwa taifa hilo hapo baadaye.Picha: dpa

Serikali ya Ujerumani jana Jumapili ilianza siku mbili za majadiliano ya ndani ya baraza la mawaziri katika ofisi ya kansela. Muungano wa vyama vya CDU, CSU na FDP unataka hadi leo Jumatatu mchana kuamua vipi serikali yao inayobeba mzigo mkubwa wa madeni inaweza kufanya mabadiliko. Kwa muda wa siku kadha kumekuwa na uvumi kuhusu wapi serikali inaweza kupunguza matumizi na iwapo itapandisha kodi.

Kansela Merkel akiwa na shauku kubwa , kwa upande wake yuko makamu wa kansela na waziri wa mambo ya kigeni , pamoja na waziri wa fedha ambaye ana mtazamo ulio halisi. Kwa hiyo, kansela Angela Merkel ,Guido Westerwelle na Wolfgang Schäuble mwanzoni mwa kikao hicho cha kubana matumizi waliwasilisha mapendekezo yao katika kikao kilichofanyika katika ofisi ya kansela. Hali ya kuvuta pumzi imezagaa, ama serikali hii takriban ndivyo inavyotamani. Katika wiki na miezi iliyopita kumekuwa na taarifa zisizopendeza, sasa kunahitajika muwafaka na nia.

Kikao hiki cha baraza la mawaziri ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya jamhuri yetu ya Ujerumani katika miaka ijayo. Uamuzi utakuwa kwa ajili ya miaka ijayo.

Ukweli ni kwamba muungano unaounda serikali unalazimika hadi mwaka 2016 kila mwaka kuziba pengo katika bajeti ya serekali kwa kiasi cha Euro bilioni nane. Ni vipi inaweza kutekeleza hilo, wataalamu wamekuwa wakilijadili hilo. Kumekuwa na uvumi hapa na pale kuhusu kile kilichokuwa sahihi ama la na hilo litafahamika leo mchana. Mwenyekiti wa chama cha FDP ambaye pia ni waziri wa mambo ya kigeni, Guido Westerwelle , anaona kuwa watendaji wa masoko ya fedha wanapaswa kubeba gharama za kuupatia ufumbuzi mzozo huu na kwamba iko nafasi ya kunusurika , makampuni ya nishati yatapaswa kutozwa kodi kwa ajili ya kurefushiwa muda wa kuendelea kutumia vinu vya kinyuklia.

Mbali ya hayo, anaweka wazi kwamba muda uliowekwa unapaswa kufupishwa.

Kazi itakuwa ni utaratibu wa kuzipata fedha na sio kinyume chake pamoja na muda ambao kiwango cha siasa iliyokuwa inatumika nchini Ujerumani ni lazima kidhibitiwe. Sifahamu , iwapo utaratibu wa kubana matumizi ambao tunajaribu kuupata hapa utapendeza kwa wapiga kura, lakini nafahamu tu kwamba hatupaswi kuliangalia suala hilo. Tunapaswa kuchukua hatua , kwa kile kilicho muhimu kwa nchi hii. Kumpendeza kila mtu ni jambo litakalopendelewa na wote, lakini tutakuwa tunajipeleka katika kugonga ukuta.

Na hata kansela Merkel anasisitiza hilo kwamba tunataka kuelekea katika wakati ambapo kutakuwa na hali bora. Kwa mtazamo huu, mtu anatambua pia kuwa suala la kupandisha kodi si jambo ambalo linapingwa mno sasa, na hata na serikali hiyo ya muungano. Pamoja na hayo, bado ni siri kwamba serikali ya mseto inaweza pia kutilia maanani suala la kupunguza mafao katika sekta ya kijamii.

ENDE