1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Serikali ya Kenya yatafakari kugawana madaraka na upinzani

11 Februari 2008
https://p.dw.com/p/D5tP

Mpatanishi mmoja wa serikali ya Kenya amesema kwa mara ya kwanza hii leo kwamba chama tawala nchi humo kinatafakari kugawana madaraka na upinzani.

Pande zinazozozana nchini Kenya zimekutana kwa mazungumzo magumu ya kujaribu kufikia makubaliano yanayolenga kuumaliza mzozo wa kisiasa nchini humo.

Wakenya wengi wamesubiri kwa hamu kubwa hii leo kusikia habari za makubaliano baada ya katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Kofi Annan, kutangaza Ijumaa iliyopita kwamba ufanisi mkubwa ulikuwa umepatikana katika kufikia makubaliano ya kugawana madaraka.