Schweinsteiger mwanasoka bora wa Ujerumani 2010
29 Desemba 2010Matangazo
Schweinsteiger, kiungo imara, alichaguliwa na jarida maarufu la michezo nchini Ujerumani, Kicker, kuwa mwanasoka bora kabisa katika mwaka 2010.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 alikuwa miongoni mwa wachezaji waliochomoza na kuonesha kandanda la hali juu katika fainali za kombe la dunia mwaka huu nchini Afrika Kusini, ambapo Ujerumani ilifikia nusufainali.
Amecheza mechi 223 katika ligi ya Ujerumani, Bundesliga, na ameshinda ubingwa wa ligi hiyo mara tano pamoja na kombe la shirikisho la soka la Ujerumani tokea alipojiunga na Bayern Munich mwaka 1998.
Mwandishi:Aboubakary Liongo/DPA
Mhariri:Othman Miradji