1. Nenda kwenye maudhui
  2. Nenda kwenye orodha kuu
  3. Nenda tovuti zaidi za DW

Sauti za wapinzani zasikika tena Iran

22 Desemba 2009

Ulrich Pick katika uchambuzi wake ufuatao anasema,mazishi ya kiongozi mkuu wa kidini Ali Montazeri ulikuwa ni wakati mwafaka wa upinzani kujitokeza tena dhidi ya utawala wa rais Mahmoud Ahmedinejad.

https://p.dw.com/p/LAa5
Maelfu ya wairan wanaopigania mageuzi,katika maziko ya Ayatollah Ali MontazeriPicha: AP

Upinzani nchini Iran ulitumia siku ya mazishi ya kiongozi wa kidini na mwanasiasa mpiganiaji wa mageuzi, Ayatollah Hossein Ali Montaseri, kuandamana. Baada ya kutolewa habari katika mtandao wa upinzani, maelfu ya wafuasi wa kiongozi huyo wa kidini walijitokeza kumsindikiza katika safari yake ya mwisho. Maafisa wa polisi walikuwa tayari kukabiliana na maandamano ya fujo ya wafuasi waliokuwa wakipiga kelele za kumpinga rais Ahmedinejad.Vyombo vya habari vya kimataifa pia vilizuia na serikali ya Iran kuripoti juu ya tukio hilo.Upinzani nchini Iran bado una nguvu na unatumia wakati kama huo ambao ni nandra ,kuandamana kuipinga serikali.

Nchini Ujerumani mtu anaposikia kuhusu upinzani nchini Iran kinachomjia katika fikra zake ni kwamba katika wakati huu nchi hiyo iko kwenye hali isokuwa tulivu. Wengi wa watu wanaofuatilia hali ya kisiasa ya taifa hilo bado wanakumbuka machoni mwao picha zilizokuwa zikionekana katika mwezi wa Juni,wakati maelfu ya wafuasi wa upinzani walipojitokeza kupinga matokeo ya uchaguzi wanaodai ulikuwa wa udanganyifu. Naam hadi wakati huu ambapo ni takriban nusu mwaka baada ya tukio hilo bado upinzani unapiga kelele na kuandamana kupinga hali hiyo. Nani ataweza kutoa hukumu juu ya hali ya sasa nchini Iran,bila shaka hilo haliwezi kupimwa kwa kuzingatia viwango vya Ujerumani. Jamhuri ya kiislamu ya Iran haiwezi hata kulinganishwa na hali ya kidemokrasia katika nchi yoyote ya ulaya ya kati. Na hiyo ndio sababu vuguvugu la kijani linaloongozwa Mir Hossein Mossavi na Mehdi Karrubi yanabidi kuwa waangalifu ili kuepuka kujitumbukiza katika makabiliano ya moja kwa moja na utawala.Tangu kuanza kwa maandamano ya upinzani nchini humo wakati wa kipindi cha joto zaidi ya maprofesa wawili wa vyuo vikuu wameuwawa,na zaidi ya watu 80 waliohusishwa na upinzani wameuwawa nchini humo.

Kufuatia hali ngumu ya kisiasa na demokrasia nchini Iran watu hujitokeza tu kuandamana wazi wazi bila ya kuwa na mashaka ikiwa hali inaonekana kuwa sio ya hatari sana kwao ya kupata mkongoto. Hivyo ni kusema kwamba,wapinzani huingia mitaani kuandamana wakati maandamano yanapoitishwa na serikali, kwa mfano dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Tehran au kupinga kukaliwa kwa Jerusalem Mashariki.

Na bila shaka shughuli ya mazishi ya kiongozi wa mapinduzi ya kiislamu Hossein Ali Montazeri pia ilitumiwa na wapinzani kupaza sauti zao bila ya kuwa na uoaga,kitisho cha kupewa mkongoto kilikuwa hakipo kwasababu Montazeri alikuwa mtu maarufu ndani ya mfumo wa vigogo waliokuwa wakiukosoa utawala .Na hivyo basi maelfu ya Wairani walijitokeza kumpa heshima ya mwisho kiongozi huyo mkuu wa kidini na wengine alau wakapata nafasi ya kuuonyesha ulimwengu kwamba bado upinzani una nguvu nchini Iran.Kifo cha Montazeri bila shaka kimesadifu kutokea katika mwezi muhimu sana wa maombolezi ya mwezi wa Muharram, ambapo kilele chake kutafikiwa jumapili ijayo katika sherehe za Ashura.Katika enzi za utawala wa Shah,kulitokea mapambano kadhaa ya utumiaji nguvu kati ya majeshi ya serikali na waandamanaji.Yawezekana jambo hili likatokea tena.Hisia katika nchi hiyo zinamfanya kila mtu kuhofia juu ya kutokea hali hiyo.

Mwandishi-Pick Ulrich/Saumu Mwasimba

Mhariri Othamn Miraji