1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

ROME: Maiti za wahamiaji zagunduliwa baharini

Walinzi wa pwani nchini Italia wamesema,maiti za watu 14 waliojaribu kuingia Ulaya kinyume na sheria zimeonekana zikiielea baharini,nje ya mwambao wa kisiwa cha Lampedusa.

Eneo la kusini ya Italia na kisiwa cha Malta hukabiliana na mfuriko wa wahamiaji wanaojaribu kuingia nchi za Umoja wa Ulaya.Siku ya Jumanne pekee,zaidi ya watu 100 waliojaribu kuingia Ulaya kwa njia za haramu,waligunduliwa nje ya kisiwa cha Lampedusa kilicho karibu ya bara Afrika kuliko Italia.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com