Roma: Maandamano Italy kupinga kupanuliwa kituo cha kijeshi cha Kimarekani nchini humo. | Habari za Ulimwengu | DW | 18.02.2007
  1. Inhalt
  2. Navigation
  3. Weitere Inhalte
  4. Metanavigation
  5. Suche
  6. Choose from 30 Languages

Habari za Ulimwengu

Roma: Maandamano Italy kupinga kupanuliwa kituo cha kijeshi cha Kimarekani nchini humo.

Maelfu ya watu waliandamana katika mji wa Vicenza, kaskazini ya Italy, wakipinga kupanuliwa kituo cha jeshi la Marekani katika eneo hilo. Watu wenye siasa za mrengo wa shoto waliompigia kura waziri mkuu Romano Prodi mwaka jana wanatuhumu kwamba amewadanganya kwa vile ameikubalia mipango ya Marekani ya kukipanua kituo hicho. Bwana Prodi anadai uamuzi huo ulikuwa umeshakamilishwa na mtangulizi wake, Silvio Berlusconi. Hakujatokea michafuko katika maandamano hayo. Ubalozi wa Marekani umwaonya raia wao wauepuke mji huo wa Vicenza.

Sikiliza Matangazo Yetu

Unaweza kusikiliza matangazo yetu hapa

Kusikiliza matangazo ya Idhaa ya Kiswahili ya DW, tafadhali bonyeza alama ya spika ya masikioni hapo chini, na kuwasiliana nasi, tafadhali tuandikie moja kwa moja kupitia: kiswahili@dw.com